Mazungumzo mengine kati ya Marekani na Urusi yanaweza kufanyika Jumapili

Utawala wa Kremlin umesema mazungumzo mengine kati ya Marekani na Urusi yanaweza kufanyika Jumapili ya wiki hii au wiki ijayo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Tangazo na Urusi limekuja wakati huu ambapo Washington ikitarajiwa pia kufanya mazungumzo na Kyiv nchini Saudi Arabia katika siku zijazo.

Rais wa Marekani Donald Trump alizungumza na rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky mapema wiki hii.

Mapema Alhamis rais Zelensky alisema kwamba Kyiv na Marekani zilikuwa zikipanga kukutana katika siku zijazo nchini Saudi Arabia.

Haijawekwa wazi iwapo maofisa wa Marekani watakutana na ujumbe wa Urusi na Ukraine katika siku hiyo.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky AFP – MIKHAIL METZEL,SERGEI SUPINSKY

Aidha haijabainika pia iwapo kunaweza kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja ambapo Moscow na Kyiv zitakuwa kwenye meza moja ya majadiliano.

Rais Putin alitupilia mbali mapendekezo ya Israel ya kusitisha vita nchini Ukraine bila ya marsharti, akikubali tu usitishaji wa mashambulio kwa kipindi cha siku 30 dhidi ya miundombinu ya nishati ya Kyiv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *