Mazungumzo kati ya Ukrainena Urusi: “Mabadilishano makubwa” ya wafungwa lakini hakuna suluhu

Wakikutana siku ya Ijumaa, Mei 16, huko Istanbul kwa mazungumzo yao ya kwanza ya amani tangu msimu wa 2022, wajumbe wa Urusi na wakle wa Ukraine wamejadili kuhusu mkutano kati ya Zelensky na Putin na kukubaliana juu ya kubadilishana kwa wafungwa, lakini sio kusitisha mapigano.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa kukosekana kwa marais Volodymyr Zelensky na Vladimir Putin, matumaini kwamba wajumbe wa Urusi na Ukraine waliotumwa Istanbul wangechukua hatua zozote kuelekea usitishaji vita wa kudumu ulikuwa mdogo. Marekani “haina matarajio makubwa,” alikiri Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio siku ya Alhamisi jioni, huku Donald Trump akisema “hakuna kitakachofanyika” hadi atakapokutana na mwenzake wa Urusi. Mkutano kama huo “ni muhimu,” Kremlin ilikiri siku ya Ijumaa.

Wajumbe hao kutoka nchi hizi mbili, wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi wa Ukraine na mshauri mkuu wa rais kwa upande wa Urusi, walikutana kwa takriban saa moja na dakika arobaini, wakiwa wamezungukwa na wapatanishi wa Uturuki, kwenye Jumba la Dolmabahçe. Mkutano huo ulimalizika bila tangazo la kusitisha mapigano, licha ya hili lilikuwa “kipaumbele” kwa Kyiv na washirika wake. Pande zote mbili sasa lazima “ziwasilishe” na “kwa undani” “maono” yao ya makubaliano kama hayo, mpatanishi wa Urusi Vladimir Medinsky amesema katika hotuba fupi kwa waandishi wa habari.

Hata hivyo, wajumbe wa Ukraine na wale wa Urusi wametangaza kwamba wamekubali kubadilishana wafungwa wa “idadi kubwa”, mshauri wa Vladimir Putin mesema, “kwa kiwango cha 1,000 kwa 1,000,” na hii “katika siku zijazo.” “Matokeo mazuri,” amesema Georgiy Tykhy, msemaji wa diplomasia ya Ukraine. Wakuu wa wajumbe wote wawili wamefafanua kwamba upande wa Ukraine pia ulijadili uwezekano wa mkutano kati ya Marais Volodymyr Zelensky na Vladimir Putin – ambao ungekuwa wa kwanza tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi – na mjumbe wa Urusi akisema tu kwamba Moscow “imezingatia ombi hili.” Hii lazima iwe “hatua inayofuata,” mjumbe wa Ukraine amebainisha kwa waandishi wa habari.

Mahitaji ya juu zaidi yanachukuliwa kuwa “hayakubaliki”

Kwa upande wa Ukraine, chanzo cha kidiplomasia kilichohojiwa na shirika la habari la AFP kimesema kwamba wajumbe wa Urusi “wamewasilisha madai yasiyokubalika ambayo yanaenda zaidi ya yale yaliyojadiliwa kabla ya mkutano,” ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa vikosi vya Kyiv kutoka “sehemu kubwa za eneo la Ukraine” kabla ya usitishaji mapigano uliotakwa na Ukraine na washirika wake kuanzishwa. Akizungumza na waandishi wa habari, Georgiy Tykhy amehakikisha kwamba timu ya Kyiv imeweza kukaa “kimya” wakati wa mazungumzo hayo. Kabla ya mkutano huo, Vladimir Medinsky amesisitiza kwamba Moscow ilitaka kujadili “sababu kuu” za mzozo huo na kuzingatia mazungumzo haya kama “mwendelezo” wa yale yaliyoahirishwa mnamo mwaka 2022, wakati Urusi ilikuwa  imeshikilia misimamo hii katika kiwango cha juu, isiyokubalika kwa Kyiv na washirika wake.

Akiwa Albania kwenye mkutano wa kilele wa Ulaya, Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa washirika wake kwa “majibu makali” na “vikwazo” dhidi ya Moscow ikiwa mazungumzo hayatafanikiwa. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameona kuwa “haikubaliki” kwamba Urusi haikuitikia vyema wito wa kusitisha mapigano, wakati Kansela Friedrich Merz amekaribisha hatua hiyo akisema kuwa mazungumzo yalikuwa yakifanyika kama “ishara ya kwanza, ndogo lakini nzuri.” Viongozi wa Ukraine, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Poland kisha wamezungumza kwa simu na Rais wa Marekani Donald Trump.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Vladimir Putin alishangaza kila mtu kwa kupendekeza mazungumzo ya moja kwa moja na Kyiv. Hata hivyo, akipingwa na Volodymyr Zelensky kwenda Istanbul kufanya mazungumzo naye, rais wa Urusi hakufanya safari hiyo. Kyiv, washirika wake wa Ulaya na Washington walikuwa wamempa Vladimir Putin kauli ya mwisho: kukubali usitishaji mapigano kabla ya majadiliano, au kukabiliwa na vikwazo “vikubwa”. Ombi lililokataliwa na Vladimir Putin, kwa msingi kwamba makubaliano ya muda mrefu yangeruhusu jeshi la Ukraine kujiimarisha kwa kupokea silaha kutoka nchi za Magharibi, wakati wanajeshi wa Urusi wana endelea kufanya vizuri kwenye mstari wa mbele na bado wanashikilia karibu 20% ya eneo la Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *