
Siku mia moja baada ya kuwasili katika Ikulu ya White House, vitendo vya Donald Trump barani Afrika vinazidi kuonekana. Na ni katika eneo la Maziwa Makuu ambapo mkakati wake unaonekana wazi zaidi. Mambo yameongezeka sana katika wiki za hivi karibuni, haswa kwa ziara ya mjumbe wake maalum kwa Afrika, Massad Boulos katika mji wa Kinshasa mapema mwezi Aprili.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Mbali na Massad Boulos, mjumbe maalum wa Donald Trump kwa Afrika yuko Corina Sanders, naibu katibu msaidizi wa masuala ya Afrika. Kwake, mkakati uko wazi: kuchanganya utulivu wa kikanda na maslahi ya kiuchumi ya Marekani, Kongo na Rwanda.
DRC ndio kitovu cha mbinu hii. Nchi ina utajiri mkubwa wa madini ya kimkakati-tantalum, niobium, tungsten, ardhi adimu, dhahabu-yaliyo hasa katika mikoa miwili ya Kivu, eneo lisilo na utulivu linalotawaliwa na uchimbaji wa madini na makundi yasiyo rasmi ambayo mara nyingi huhusishwa na kampuni za Kichina na magendo yanayohusishwa na nchi jirani.
Nyuma ya lengo la amani, juu ya yote ni suala la kufungua njia kwa uwekezaji wa Marekani katika eneo la kimkakati. Masuala matatu yanaongoza mashambulizi ya Trump: kupata upatikanaji wa madini muhimu dhidi ya China, kuleta utulivu mashariki mwa Kongo ili kuvutia mitaji, na kuimarisha uwepo wa Marekani kupitia Minerals Security Partnership Forum. Kazi hii tayari ilikuwa imeanza kusini zaidi, huko Katanga, na ukanda wa reli ya Lobito. Lakini wazo la kupanua mhimili huu hadi Mashariki lilikutana, kulingana na Washington, upinzani kutoka kwa Rwanda.
Ni kwa mantiki hiyo ndipo kutiwa saini kwa tamko la kanuni kati ya DRC na Rwanda,zoezi lililofanyika Washington, chini ya upatanishi wa Marekani: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Rwanda zilitia saini, siku ya Ijumaa, Aprili 25, mjini Washington, tamko la kanuni lililowasilishwa kama hatua muhimu katika kuanzishwa upya kwa mchakato wa amani.
Katika andiko hili, Rwanda na DRC ziliweka makataa ya kufikia rasimu ya makubaliano ya amani, na kujitolea kupendelea njia za kidiplomasia badala ya kutumia silaha kutatua mzozo wao. Ili kufikia hili, masuala ya usalama yatahitaji kushughulikiwa ndani ya tume ya utaratibu. Nchi hizo mbili pia zinajitolea kwa kanuni mbalimbali kama vile kutambua uadilifu wa eneo na mipaka ya kila mmoja wao, umuhimu wa kuzuia kuenea kwa makundi yenye silaha yasiyo ya serikali na kurejea kwa hiari kwa wakimbizi na maelfu ya wakimbizi wa ndani, huku pia wakitambua jukumu la MONUSCO.
Rais wa Kongo Félix Tshisekedi aelezea imani yake
Siku tatu baada ya kutiwa saini Washington kwa tamko la kanuni kati ya DRC na Rwanda, rais Félix Tshisekedi alikaribisha hatua kubwa ya kusonga mbele kuelekea amani. Siku ya Jumanne mjini Kinshasa, wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na mwenzake kutoka Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo, mjini Kinshasa, mkuu wa nchi wa Kongo alithibitisha ahadi yake.
Ni kauli ya kanuni, ni kweli, ni hatua katika mwelekeo sahihi, mwelekeo ambao siku zote nilitaka kuutoa kwa nchi yangu, na nilitoa ahadi hii mbele ya watu wangu. Nitaishikilia hadi mwisho. Nitarudisha amani, lakini amani ya kweli na ya kudumu. Baadaye… hakutakuwa tena na matatizo ya ukosefu wa utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hayo ni matakwa yangu na kiapo changu. Na sitasema zaidi… Na niwakupa miadi tu siku ambayo amani hii itatimia. Haya basi, asante.