Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za AES waanza ziara nchini Urusi

Mawaziri wa mambo ya nje wa Mali, Niger, na Burkina Faso walianza ziara nchini Moscow siku ya Jumatano kwa mwaliko wa mwenzao wa Urusi, Sergei Lavrov. Mkutano huu, unaoitwa “kikao cha kwanza cha mashauriano ya Muungano wa Nchi za Sahel (AES) – nchini Urusi,” unalenga kuimarisha uhusiano kati ya Moscow na nchi hizi tatu zinazoongozwa na wanajeshi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu katika kanda, Serge Daniel 

Washirika wakuu wa Russia, Mali, Niger na Burkina Faso, wataikumbusha Moscow kwamba usalama katika Sahel unasalia kuwa kipaumbele chao kikuu. Kwa mujibu wa habari zetu, maafisa wanaohusika na masuala ya ulinzi na usalama ni miongoni mwa mafisa hao wanaofanya ujumbe kutoka nchi hizo tatu.

Mwenyeji wa mkutano pia atazihakikishia nchi hizi tatu zinazoongozwa na tawala za kijeshi ambazo ni wanachama wa Muungano wa Nchi za Sahel (AES). Iwe chini ya lebo ya kundi la wanamgambo la Wagner, chini ya jina jipya, au kupitia ushirikiano rasmi, Urusi inakusudia kuimarisha uhusiano wake na Mali, Niger na Burkina Faso. Nchi hizi tatu zinatangaza kuundwa kwa muungano wa pamoja wa ulinzi.

Katika ziara hiyo ya saa 48 nchini Urusi, masuala ya kiuchumi pia yatakuwa mezani kujadiliwa. Mojawapo ya miradi kuu ya Muungano wa Nchi za Sahel (AES) ni uundaji wa hivi majuzi wa benki ya kikanda ya uwekezaji. Mwanzo wa taasisi ya fedha ulikuwa wa uvivu. Ushirikiano na Moscow utaombwa.

Katika eneo jingine, diplomasia, pande hizo mbili zinaweza kufafanua mfumo ili kuzungumza kwa ngazi ya kimataifa kwa sauti moja katika masuala kadhaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *