Mauaji ya mtoto Samantha Pendo: Ukatili wa polisi na muda mrefu wa kusubiri haki nchini Kenya

Familia hiyo inaishi mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya- ngome ya upinzani ambako ghasia zilizuka Agosti 2017 kuhusu matokeo ya uchaguzi ambao hatimaye ulirudiwa kwa sababu ya dosari.