Mauaji ya Kimbari Rwanda: Agathe Habyarimana, mjane wa rais wa zamani wa Rwanda kuchunguzwa

Hii ni hatua mpya katika kesi za kisheria dhidi ya Agathe Habyarimana nchini Ufaransa. Mahakama ya Rufaa ya Paris imechunguza, Jumatano, Machi 19, ombi kutoka kwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa taifa wa Kupambana na Ugaidi (PNAT) inayoomba kuwa mwa rais wa zamani wa Rwanda ashtakiwe kwa “njama ya kufanya mauaji ya halaiki.”

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Rufaa ya Paris haikuweza kuzingatia maombi ya mwendesha mashtaka wa umma. Kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa kwa faragha siku ya Jumatano, Machi 19, haikuweza kufanyika kwa sababu nyaraka mbalimbali zinazohitajika na Mahakama ya Rufaa, ikiwamo majarida, hazijawasilishwa kikamilifu. Kwa hiyo kesi mpya imepangwa kufanyika Mei 21, 2025. Agathe Habyarimana, mjane wa Rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana, ambaye mauaji yake yalisababisha mauaji ya kimbari ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, alipelekwa uhamishoni Paris tangu kuanza kwa mauaji hayo. Bado yuko Paris, lakini familia za wahasiriwa ambao wanamshtumu kwa jukumu lake katika kundi la vigogo wa Kihutu wenye msimamo mkali zaidi waliokuwepo Kigali wakati huo.

Uchunguzi umekuwa wazi tangu malalamiko yaliyowasilishwa mwaka 2007 na muungano wa vyama vya kiraia nchini Rwanda. Mawakili wa Agathe Habyarimana wanabaini kwamba kesi hii ni tupu, ni ya kisiasa na kwamba kesi hiyo inapaswa kufutwa.

Mahakama ya Rufaa ya Paris inapaswa kutoa uamuzi kuhusu maombi matatu kutoka kwa mwendesha mashtaka wa umma: kushtakiwa kwa Agathe Habyarimana kwa kula njama ya kutekeleza mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu, kurefushwa kwa uchunguzi huo kuanzia Machi 1, 1994, badala ya siku tatu zinazozunguka kuzuka kwa mauaji ya halaiki, na uchunguzi mpya.

“Hatua muhimu” katika taratibu za ufunguaji kesi za kisheria 

Kwa muungano wa vyama vya kiraia nchini Rwanda, chini ya uenyekiti wa Alain Gauthier, ambaye alianzisha malalamiko dhidi ya mke wa rais wa zamani mwaka wa 2007, unasema maombi haya ni ya msingi ili kuruhusu uchunguzi kuendelea. “Ni muhimu, ni hatua muhimu ikiwa tunataka kesi iendelee. Ikiwa upande wa mashtaka unaomba shtaka, ni kwa sababu wana ushahidi, sio kumfurahisha mtu yeyote. “Kwetu sisi, muhimu ni wahasiriwa, sio mamlaka ya Kigali,” anafafanua. 

Akiwa chini ya hadhi ya shahidi aliyesaidiwa mwaka 2016, Agathe Habyarimana alisikilizwa tena na jaji mnamo mwezi Desemba 2024. Mwanasheria wa Agathe Habyarimana, Wakili Philippe Meilhac, ambaye anaona kuwa kufutwa kwa kesi hiyo kulipaswa kutangazwa mwaka wa 2022 kutokana na ukosefu wa ushahidi, anabaini kwamba maombi ya mwendesha mashtaka wa umma juu ya yote yanawezesha kuweka utaratibu wazi, na kwa hiyo, sio kuudhi mamlaka ya Rwanda: 

“Kesi hii iko tupu kwa mteja wangu ambaye anasumbuliwa nayo. Mchezo wa upande wa mashtaka uko tupu kabisa. Yote ni ujanja halisi wa kisheria. Lengo ni kuchelewesha wakati ambapo kufutwa huku kwa kesi hii kutaamriwa kwa mazingatio ya kisiasa. »Agathe Habyarimana mwenye umri wa miaka 82 hatakuwepo kwenye kesi hiyo. Uamuzi wa chumba cha uchunguzi utahifadhiwa, kama inavyotakiwa na utaratibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *