Mauaji katika msikiti Ufaransa: Mshukiwa aliyekamatwa nchini Italia, ‘lijisalimisha mwenyewe’

Muuaji wa kijana kutoka nchini Mali katika msikiti ulioko kusini mwa Ufaransa, ambaye alimpiga picha mwathiriwa baada ya kutekeleza ukatili wake huo siku ya Ijumaa, alikamatwa baada ya “kujisalimisha” katika kituo cha polisi nchini Italia, mwendesha mashtaka wa Ufaransa anayesimamia kesi hiyo ametangaza siku ya Jumatatu, Aprili 28.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

“Ninaridhika sana kama mwendesha mashtaka. “Kutokana na ufanisi wa hatua zilizowekwa, mhusika hakuwa na chaguo ila kujisalimisha, na hilo ndilo jambo bora zaidi ambalo angeweza kufanya,” ameongeza kwa simu.

Kutokana na kukamatwa kwake nchini Italia, jaji wa uchunguzi “atafahamishwa” na hati ya kukamatwa ya nchi za Umoja wa Ulaya iliyotolewa kwa nia ya uhamisho wake kwenda Ufaransa, amebainisha. Zaidi ya maafisa 70 wa polisi wa Ufaransa na askari wamehamasishwa tangu Ijumaa “kumtafuta na kumkamata” mtu huyu, anayechukuliwa kuwa “hatari sana,” kulingana na mwendesha mashtaka.

“Baada ya kujivunia kitendo chake, baada ya kudai kuhusika na kitendo hicho, alitoa maoni ambayo yangependekeza kuwa alikusudia kufanya vitendo kama hivyo tena,” mwendesha mashtaka alibainisha siku ya Jumapili.

“Chini ya rada ya haki”

Maelezo yaliyotolewa rasmi kuhusu mshukiwa, ambaye mwenyewe alirekodi mauaji hayo, yalibakia kuwa machache: Olivier A. anatoka katika familia ya Bosnia, hana kazi, akiwa na uhusiano na Gard, idara ambayo mauaji yalifanyika, katika mji wa La Grande-Combe. 

“Ni mtu ambaye alikuwa akifuatiliwa na mahakama pamoja na polisi na ambaye, wakati wowote, alikuwa amezungumziwa hadi matukio haya ya kutisha kutokea,” Abdelkrim Grini alieleza siku ya Jumapili.

Huko La Grand-Combe, maandamano ya kimyakimya ya kumkumbuka mwathiriwa, Aboubakar Cissé, raia wa Mali mwenye umri wa miaka ishirini, yaliwaleta pamoja zaidi ya watu elfu moja siku ya Jumapili alasiri, kati ya msikiti wa Khadidja, ambapo mkasa huo ulitokea, na makao makuu ya mji wa mji huu mdogo wenye wakazi wasiozidi 5,000.

Mamia kadhaa ya watu pia walikusanyika mjini Paris mapema jioni, akiwemo kiongozi wa chama chenye siasa kali za mrengo wa kushoto cha La France Insoumise, Jean-Luc Mélenchon, ambaye alimshutumu Waziri wa Mambo ya Ndani Bruno Retailleau kwa kuchochea  “hali ya chuki dhidi ya Uislamu.”

“Ubaguzi wa rangi na chuki zinazoegemezwa kwenye misingi ya dini hazitawahi kuwa na nafasi nchini Ufaransa,” Rais Emmanuel Macron alihakikisha siku ya Jumapili mchana, akielezea ” serikali na wananchi wanaungana na familia ya mwathiriwa na “wenzetu wa imani ya Kiislamu” kwa kuomboleza kifo cha kijana huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *