Matukio ya chuki dhidi ya Waislamu UK yamevunja rekodi 2024 kutokana na vita vya Israel Ghaza

Idadi ya matukio na vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu nchini Uingereza iliongezeka kufikia kiwango cha zaidi mwaka 2024. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na shirika la ufuatiliaji la Tell MAMA, ambalo limesema vita vya Ghaza “vimechochea kupita kiasi” masuala ya chuki dhidi ya Waislamu kwenye mitandao ya kijamii.