Mateka wa Kizayuni: Kwa muda wote walipotushikilia, Al-Qassam waliamiliana nasi kwa wema

Gazeti moja la Kizayuni limemnukuu mateka mmoja Muisrael akisema kuwa Wanamuqawama wa Brigedi za al-Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya HAMAS waliamiliana kwa wema na mateka hao wa Kizayuni kwa muda wote walipokuwa wakiwashikilia huko Ukanda wa Ghaza.