Mashtaka dhidi ya utawala wa Biden katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu

Taasisi ya “Demokrasia kwa ajili ya Ulimwengu wa Kiarabu Sasa” (DAWN), imefungua mashtaka dhidi ya Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden na mawaziri wake wawili yaani waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Anthony Blinken na waziri wa zamani wa ulinzi wa nchi hiyo Lloyd Austin katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ikiitaka ianzishe uchunguzi dhidi ya viongozi hao kutokana na kusaidia uhalifu wa kivita wa utawala wa Kizayuni wa Israel.