Mashirika ya kibinadamu yanatafuta dola bilioni 1.4 kwa ajili ya Somalia kwa mwaka huu wa 2025

Umoja wa Mataifa na washirika wa misaada ya kibinadamu jana Jumatano walizindua Mpango wa Mahitaji ya Kibinadamu wa 2025 (HNRP), ambao unalenga kukusanya dola bilioni 1.42 kusaidia watu milioni 4.6 nchini Somalia.