Mashirika ya haki za binadamu yatahadharisha kuhusu amri ya Trump ya kuwazuia Waislamu kuingia Marekani

Wanaharakati wa haki za kiraia wameitaja amri mpya ya kiutendaji iliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani inayowazuia raia wa nchi za Kiislamu kuingia Marekani kuwa ina taathira kubwa zaidi kuliko kile kilichoshuhudiwa mwaka 2017 na katika awamu ya kwanza ya serikali yake.