Mashirika nchini Rwanda yapigwa marufuku kushirikiana na Ubelgiji

Serikali ya Rwanda, imepiga marufuku mashirika yote ya ndani na kimataifa yasiyokuwa ya kiserikali kushirikiana na taasisi za Ubelgiji, baada ya nchi hizo mbili kusitisha ushirikiano wa kidiplomasia mapema mwezi huu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Bodi ya Rwanda inayoshughulikia masuala ya uongozi imesema marufuku hayo, yanaathiri pia mashirika yote ya dini pamoja na mengine yote yanayohusishwa na serikali au mashirika kutoka Ubelgiji.

Miradi yote iliyokuwa inaendelea kwa msaada wa serikali ya Ubelgiji, imesitishwa na mikataba iliyokuwa imetiwa saini, imefutwa, kwa mujibu wa maagizo ya bodi hiyo ya Rwanda.

Wakati huu wa marfuku hakuna msaada wa fedha, utakapokelewa na mashirika hayo yaliyo nchini Rwanda kutoka kwa serikali ya Ubelgiji na mashirika yake yote.

Uamuzi huu wa serikali ya Rwanda, umekosolewa vikali na mwanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu Pelly Prudence Iraguha, ambaye amesema uamuzi huo, ungepelekwa bungeni kwanza.

Rwanda ilivunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Ubelgiji Machi tarehe 17, kwa madai ya kuendelea kudharau nchi hiyo, na kuendelea kuishtumu kuhusika na mzozo wa Mashariki mwa DRC kwa kuwaunga mkono waasi wa M 23.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *