Mashauriano ya Iran na Ethiopia ya kupanua uhusiano wa kiuchumi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya Bunge amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mshauri katika Wizara ya Masuala ya Kigeni ya Ethiopia ambapo wamejadiliana njia za kupanua ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizi mbili ikiwemo uanachama katika kundi la “BRICS”.