Mashariki mwa DRC: Wanasiasa wagawanyika kuhusu uteuzi wa Rais wa Togo kama mpatanishi

Rais wa Togo Faure Gnassingbé amedokezwa kuanza tena upatanishi kati ya DRC na Rwanda. Uamuzi uliotangazwa tarehe 5 Aprili 2025 na João Lourenço, rais wa Angola na mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU), wakati wa mkutano wa mtandaoni wa ofisi ya shirika hilo.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Lourenço, ambaye alikuwa ameshikilia wadhifa huu kwa miaka miwili, alithibitisha kujiondoa kwake na akataka kuendelezwa kwa mazungumzo kati ya Kinshasa na Kigali. Huko Kinshasa, walio wengi wakaribisha hatua hiyo wakati upinzani unaonyesha kutoridhishwa kwawke.

Kambi ya waliowengi wanakaribisha hatua ya rais wa Angola na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, aliyekuwa muwezeshaji kati ya DRC na Rwanda kuhusu mgogoro mashariki mwa DRC, bila ukosoaji wa wazi. 

Lambert Mende, mbunge na mjumbe wa wa muungano wa Union Sacrée, jukwaa tawala, anaeleza kuwa kambi yake “haina hoja” dhidi ya uteuzi wa rais wa Togo: “Tunapoingia katika hali ya kupinga wasuluhishi, tuna hatari ya kutoondokana na mgogoro. Kila nchi ina changamoto zake. Angola, kwa mfano, ilikumbwa na vita vya kutisha vya wenyewe kwa wenyewe. Sio sisi kusema kuwa kama rais Gnassingbé aliweza kukutanisha pande hasimu katika nchi yake. Leo kinachohitajika, ni kuweza kuzungumza na Rwanda, nchi iliyovamia nchi yetu. Kuna hitajika msuluhishi. Je, Faure Gnassingbé ni sahihi? Rais wetu ataamua na atatwambia. “

Katika upinzani, majibu yanapimwa zaidi. Claudel-André Lubaya, mpinzani na mwanachama wa Mfumo wa Ushauri wa vikosi vya Kisiasa na Kijamii, jina la Faure Gnassingbé lina umuhimu mdogo. Kulingana naye, ikiwa Umoja wa Afrika ulipendekeza, lazima iwe na sababu zake. Lakini anaonya juu ya jambo lingine: “Ninakaribisha mipango yote ya amani. Lakini leo, mipango hiyo hutawanywa, sambamba, wakati mwingine kushindana na kwa wakati mmoja. Ushirikiano wao unaleta mkanganyiko na hutuondoa kutoka kwa suluhisho ambalo watu wanatarajia. Ni lazima haraka kurejesha uwazi na uratibu bora zaidi. ” 

Uteuzi ambao bado unahitaji kuidhinishwa na AU 

Bado inasalia hatua moja kabla ya uwezekano wa uteuzi rasmi : pendekezo kuhusu rais wa Faure Gnassingbe litaidhinishwa rasmi na mkutano mkuu wa maris na viongozi wa serikali wa Umoja wa Afrika kupitia utaratibu unaoitwai “kimya”.

Wakati huo huo, mchakato mwingine unaendelea: wajumbe kutoka kwa serikali ya Kongo na vuguvugu la wasi la AFC/M23 wanatarajiwa mjini Doha kwa duru ya pili ya mazungumzo, kama sehemu ya upatanishi unaoongozwa na Qatar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *