
Wakati hali ya mashariki mwa DRC ni kitovu cha shughuli kubwa za kidiplomasia, wanasiasa wa Kongo wanaendelea kuguswa na maendeleo ya hivi karibuni katika ngazi ya kimataifa. Mwishoni mwa juma, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakati wa mkutano wao wa pamoja walitoa wito wa usitishaji vita “mara moja na bila masharti” katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, inayokabiliwa na mapigano kati ya FARDC na M23 na washirika wake, jeshi la Rwanda.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Kutoka kwa mwanahabari wetu mjini Kinshasa,
Tangu siku ya Jumapili na mikutano ya kikanda, kumekuwa na utulivu katika maeneo ya mapigano. Lakini siku ya Jumanne asubuhi, milipuko imeripotiwa katika eneo la Kalehe katika mkoa wa Kivu Kusini. Ni mapema sana kusema ikiwa hili ni tukio la kipekee au kuanza tena kwa mapigano.
Ni vigumu kujua ukweli kuhusu usitishaji vita kwani, ingawa iliombwa mara moja, mazingira hayajawekwa sawa. mashirika haya mawili ya kikanda yamewapa wakuu wa majeshi siku tano kukutana, pengine nchini Tanzania, na kutathmini kinachotakiwa kufanywa.
Kutoa misaada
Maazimio mengine yalichukuliwa mwishoni mwa mkutano huu: shirika la misaada ya kibinadamu. Hivi sasa huko Goma, mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yanafanya kazi na kile walichokuwa nacho kabla ya mapigano, baadhi ya hifadhi zimeporwa. Kwa hivyo kufunguliwa kwa uwanja wa ndege ni dharura.
Hatimaye, wakuu wa majeshi wanapaswa pia waweke mpango wa kutoa ulinzi kwa mji wa Goma. Wakongo wengi wanasema, hii ina maana M23 kuondoka. Lakini hii pia haijafafanuliwa.
Kinshasa, wanasiasa wagawanyika kuhusu diplomasia ya serikali
Rwanda haikutajwa katika taarifa ya mwisho wa mkutano huo: hata hivyo hili lilikuwa mojawapo ya matakwa ya Kinshasa. Lakini ishara zinasalia kuwa chanya, kulingana na mamlaka ya Kongo. “Hatukwenda Dar es Salaam kumweleza mhalifu, kila mtu anamfahamu,” alisema Waziri wa Mawasiliano.
Waziri huyu wa Mambo ya Nje wa DRC alikuwa na shauku ya kukumbusha maendeleo yaliyofikiwa na diplomasia ya Kongo katika siku za hivi karibuni na haswa, kupitishwa kwa azimio katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva kwa ajili ya kuanzishwa kwa ujumbe wa uchunguzi wa uhalifu uliofanywa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini tangu mwezi Januari 2022.
Lakini upande wa upinzani, maoni yamekuwa tofauti. Kwa mujibu wa Olivier Kamitatu, msemaji wa mwanasasa wa upinzani Moïse Katumbi, hii ni hatua muhimu na usitishaji vita huu na kipengele cha kibinadamu.
lazima “tuingie katika mantiki halisi ya mazungumzo”, amesema Olivier Kamitatu, kutoka chama cha Ensemble
Kwa upande mwingine, kwa muungano wa Lamuka wa Martin Fayulu, wanasema inakatisha tamaa: “mikutano ya kilele ya kilamara, usitishaji mapigano wa kila mara, hali katika uwanja wa mapigano bado ni ile ile,” anasema msemaji wake Prince Epenge.
Kwa upande wa kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila wanaona kuwa suluhu lamzozo huu halipo tena katika “mikutano hii”. Kwa mujibu wa kiongozi wa PPRD Ferdinand Kambere, “Rais Félix Tshisekedi ameonyesha mipaka yake, lazima atambue kwamba hawezi tena kutatua mgogoro wa Mashariki.”