Mashariki mwa DRC: Wanajeshi wa SADC wameanza kuondoka Goma

Wanajeshi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliotumwa mashariki mwa DRC tangu mwezi wa Desemba 2023 wameanza kuondoka nchini humo kupitia Goma, msemaji wa SADC amethibitisha Aprili 29, 2025. Kuondoka huko kulijadiliwa na vuguvu la kisiasa la AFC/M23.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wanajeshi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wameanza kuondoka Goma mashariki mwa DRC leo Aprili 29, 2025. Kuondoka kwa waajeshi hao kulijadiliwa na kundi la kijeshi na kisiasa la AFC/M23 ambalo limedhibiti mji mkuu wa miko ya Kivu Kaskazini tangu mwisho wa mwezi wa Januari. Shirika la kikanda halikubainisha ni wanajeshi wangapi waliondoka nchini humo leo Jumanne asubuhi.

Hakuna takwimu zilizotolewa kwa sababu za usalama, msemaji wa SADC amesema. Shirika la kikanda limebainisha tu kwamba hiki ndicho kikosi cha kwanza cha SAMIRDC kuondoka Goma, mbali na wanajeshi 200 waliojeruhiwa ambao tayari walikuwa wamehamishwa mwishoni mwa mwezi wa Februari.

Watumia barabara kuondoka mashariki mwa DRC

Wanajeshi hawa waliondoka mapema leo asubuhi kwa barabara, mara tu mpaka na Rwanda kufunguliwa, msemaji wa SADC amesema. meiongeza kuwa kundi la mwisho la kikosi hiki cha kijeshi litaondoka mwishoni mwa mwezi wa Juni.

Idadi ya wanajeshi wa SAMIRDC walioondoka haijatangazwa, lakini wachambuzi wanakadiria ni karibu wanajeshi 1,300. Kikosi hiki kinaundwa na wanajeshi kutoka Afrika Kusini, Malawi na Tanzania, kimetumwa tangu mwezi Desemba 2023 kusaidia jeshi la Kongo na kuzuia kusonga mbele kwa M23.

Tangu waasi hao wachukue udhibiti wa Goma, wanajeshi wa SAMIRDC wamekimbilia katika kambi ya Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) huko Goma, bila hata hivyo kuondoka katika kambi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *