
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, shughuli za masomo zilianza tena kwa hofu siku ya Jumatatu Februari 10 huko Goma, zaidi ya wiki mbili baada ya kuanza kwa mapigano kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda. Lakini wanafunzi wengi hawakuenda shule: baadhi ya shule zilizoporwa au kuharibiwa, haziko katika hali ya kuanza tena masomo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Katika shule za msingi za Majengo na Totoro, kama ilivyo katika shule nyingi za Goma, kilio cha watoto hakisikiki. Milango ya madarasa imeendeea kufungwa. Hapa, walimu pekee waliripoti shuleni, kwa sababu wazazi wa wanafunzi bado wana mshtuko.
“Sikuwapeleka watoto shule kwa sababu najua hali ilivyo, jiji halijawa shwari tena,” analalamika mzazi mmoja. Wakati mamlaka zilizopo zinaweza kutuhakikishia kwamba hakutakuwa na tatizo, basi tunaweza kuwarudisha watoto wetu shuleni.”
“Watoto wangu hawakwenda shule leo kwa sababu wanaogopa, hawajawahi kuishi katka mazingira ya kivita na wanaogopa vilipuzi,” anaeleza mama mmoja.
Licha ya hofu hizi, Justin Muganzi, mkuu wa shule ya msingi, anajaribu kuwashawishi wazazi: “Hakuna mwanafunzi aliyejitokeza shuleni. Ujumbe ni kwamba tunawafahamisha wazazi juu ya hitaji la kuwaleta watoto wao shuleni. “
Kila kitu kiliporwa
Upande wa magharibi wa Goma, shule ya Cinquantenaire, mojawapo ya shule maarufu zaidi jijini, imepoteza mng’ao wake: ubao katika kila darasa, milango, madawati, kila kitu kimeporwa. Shule inaonekana katika mfumo wake wa zaani wakati ilipoanza kujengwa. Élie Kayenga, mwalimu wa Kifaransa, analalamika: “Tulipaswa kuanza kama wengine. Lakini kama unavyoona, madarasa yote ni tupu. Hakuna meza, hakuna kiti, hakuna ubao. Kuandaa madarasa haya yote haitakuwa rahisi kwa shule, ambayo haina chochote. Inasikitisha. “
Mwishoni mwa wiki, mamlaka ya jimbo la Kivu Kaskazini kutoka serikali ya DRC na waasi wa M23 walitoa wito wa kuanza kwa masomo.