
Mwezi mmoja baada ya kusitishwa mara moja kwa mapigano mashariki mwa DRC na kuondolewa kwa vikosi vya Rwanda, vilivyotakwa na Umoja wa Mataifa kwa kura ya azimio 27-73, Baraza la Usalama lilikutana tena jana, Alhamisi, kutambua maendeleo kutokana na ripoti ya Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa MONUSCO.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini New York, Carrie Nooten
Wakati hali ya usalama na kibinadamu ikizidi kuwa mbaya, Baraza limetangaza nia yake ya kuona suluhu ya kisiasa ikiibuka. Mjini New York, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda amekanusha kuhusika kikamilifu kwa wanajeshi wa Rwanda na kuishambulia kwa nguvu MONUSCO.
Tangu mwezi uliopita, vuguvugu la AFC/M23 wameteka sehemu kubwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini na mkoa wa Kivu Kusini. Mkuu wa MONUSCO anaamini kuwa mikoa ya Maniema na Tshopo ndiyo lengo lao linalofuata. Pia ameelezea hali ya kibinadamu ambayo inazidi kuwa mbaya kutokana na mfumo wa benki kutokuwa mzuri na miundombinu duni inayozuia utoaji wa chakula. Ametoa wito wa kufunguliwa tena kwa viwanja vya ndege vya Goma na Kavumu.
Mabalozi wa DRC, Angola na Burundi, kama Baraza zima, wametoa wito wa mzozo huo usuluhishwe kisiasa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe amekataa kuthibitisha kwa vyombo vya habari idadi ya wanajeshi wa Rwanda waliotumwa mashariki mwa DRC.
“Nchini Rwanda, tumeweka hatua za kujihami katika mpaka wetu ili kujilinda dhidi ya vitisho vinavyotoka mashariki mwa DRC katika kipindi cha miaka 30. “Wanamgambo na makundi yanayofanya kazi na serikali ya Kinshasa na wanataka tu kupindua serikali ya Rwanda,” amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda pia ameishambulia MONUSCO, akiishutumu kwa “kupotosha ukweli wa mambo, na kuegemea upande mmoja na kushindwa kwa kazi yake kubwa ya kuvunja makundi yenye silaha nchini DRC,” licha ya Baraza kuunga mkono kwa kauli moja kikosi cha Umoja wa Mataifa.