Mashariki mwa DRC: Umoja wa Mataifa watoa wito wa mazungumzo kati ya pande husika

Katika ufunguzi wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU), Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amebainisha siku ya Jumamosi Februari 15 kwamba kuna ulazima wa kuepuka “kuongezeka kwa machafuko ya kikanda kwa gharama yoyote” na kwamba “uhuru na uadilifu wa eneo la DRC lazima uheshimiwe.” 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Saa chache baada ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kuingia katika vitongoji vya kaskazini mwa Bukavu, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa pia ametoa wito wa “mazungumzo kati ya pande zinazopigana” mashariki mwa DRC.

Umoja wa Ulaya umesema siku ya Jumamosi kwamba “unachunguza kwa dharura” chaguzi zote zinazoweza kuchukuliwa. “Ukiukaji unaoendelea wa uadilifu wa eneo la DRC hautosalia hivo bila jibu,” ameongeza Anouar El Anouni, msemaji wa EU kwa masuala ya Mambo ya Nje, kwenye X.

Kwa upande wake, diplomasia ya Ufaransa imetoa wito siku ya Jumamosi “kusitishwa mara moja” kwa mashambulizi na kutaka “kuondoka mara moja” kwa vikosi vya Rwanda vinavyounga mkono kundi hili lenye silaha linalopinga serikali ya DRC.