
Jina la rais wa Togo limependekezwa kuchukua mwenge wa upatanishi kati ya Kinshasa na Kigali wakati wa mkutano wa video wa ofisi ya Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU), Jumamosi, Aprili 5. Mkutano huo umeongozwa na João Lourenço, ambaye sasa ni rais wa Angola na mkuu wa sasa wa shirika hilo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Baada ya kueleza rasmi nia yake ya kujiondoa katika upatanishi kati ya DRC na Rwanda, ambao amekuwa akiuendesha kwa miaka miwili, wakati wa mkutano wa ofisi ya Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) Jumamosi, Aprili 5, João Lourenço amesisitiza juu ya haja ya kuhakikisha kuendelea kwa mchakato wa mazungumzo kati ya pande hizo mbili na kisha kuweka mbele jina la Faure Gnassingbé kuchukua nafasi yake.
Ingawa pendekezo hilo liliungwa mkono na wajumbe wa ofisi ya Mkutano huo na mashauriano ya awali na mtu husika yalikuwa mazuri, kwa mujibu wa mkuu wa nchi wa Angola, uteuzi wa rais wa Togo, hata hivyo, utasubiri kuthibitishwa rasmi na Bunge la Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU, kupitia utaratibu unaoitwa “kimya”.
Katika hotuba yake, Joao Lourenço pia amekaribisha maendeleo yaliyofikiwa katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao ulifanyika mwishoni mwa mwezi Machi, na kutaja kuoanishwa kwa mchakato wa Nairobi na Luanda pamoja na uteuzi wa wawezeshaji wenza watano wa Kiafrika – ambao walifanya mkutano wao wa kwanza mnamo Aprili 1.