Mashariki mwa DRC: Takriban wanajeshi 55 wanaotuhumiwa kutoroka mapigano wahukumiwa kifo

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), askari wasiopungua 55 wa Kikosi cha Wanajeshi wa Kongo (FARDC) wamehukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi siku ya Ijumaa, Februari 28. Wanajeshi hawa wanatuhumiwa kumkimbia adui wakati wa mashambulizi ya hivi punde zaidi ya kundi la M23, linaloungwa mkono na Rwanda, dhidi ya ngome za jeshi la FARDC katika eneo la Lubero, Kivu Kaskazini.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya kijeshi ya Butembo, iliyojielekeza Musienene mashariki mwa DRC, ilitoa uamuzi wake baada ya siku tano za kesihiyo kusikilizwa. Wengi wa wanajeshi wa FARDC wanaoshutumiwa kwa “woga mbele ya adui” ni maafisa wenye veo vya chini. Mashtaka dhidi yao yanaanzia kutoroka mbele ya adui hadi kupoteza silaha za kivita, pamoja na kutiwa hatiani kwa wizi, ubakaji na uporaji.

Ukatili huu ulifanyika Lubero-Center, Kimbulu, Musienene na katika mji wa Butembo. Kwa jumla, wanajeshi 55 wa jeshi la Kongo walihukumiwa kifo. Wengine sita waliachiliwa katika kesi hiyo. Kulingana na jeshi la Kongo, vikao vingine vya mahakama vitafanyika hivi karibuni, na kuonekana kwa askari wengine waliokamatwa haswa huko Beni, Oicha na kwingineko kwa makosa  kama jhayo.

Mnamo Julai 2024, karibu askari hamsini wa FARDC walikuwa tayari wamehukumiwa kifo katika kesi ya kihistoria huko Alimbongo kwa kutoroka dhidi ya M23. Eneo hilo sasa linadhibitiwa na kundi hili la wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda.