
Mashariki mwa DRC, mgodi wa bati wa Bisié, mgodi wa tatu kwa ukubwa duniani, utaanza shughuli zake hatua kwa hatua baada ya kujiondoa kwa kundi la waasi la M23 kutoka eneo la Walikale.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Shughuli katika mgodi wa bati wa Bisié inatarajiwa kuanza tena baada ya kusitishwa kwa sababu za usalama. Kampuni inayomilikiwa na Marekani Alphamin ilitangaza hatua hiyo siku ya Jumatano, Aprili 9, huku juhudi za kidiplomasia zikizidi kukomesha mzozo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kampuni hiyo inawarejesha wafanyakazi wake ili kuanza tena shughuli zake, kwa awamu, za uzalishaji wa bati huko Bisié mashariki mwa DRC. Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kujiondoa kwa kundi la AFC/M23 lililo umbali wa zaidi ya kilomita 130 kutoka Walikale, kampuni ya Alphamin imebaini katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Aprili 9, 2025.
Mnamo Machi 13, Alphamin ilitangaza kusitishwa kwa shughuli zake na kuwahamisha wafanyakazi wake kwa sababu za usalama, wakati wapiganaji wa M23 wakiungwa mkono na Rwanda walipokuwa wakikaribia mgodi huo.
Siku chache zilizopita, katika ziara yake mjini Kinshasa, mshauri wa Donald Trump wa masuala ya Afrika alithibitisha “dhamira” ya Marekani ya kumaliza mzozo huo kwa amani, wakati akijadili makubaliano ya uchimbaji madini na mamlaka ya Kongo. “Tunashukuru kwa mazungumzo yanayoendelea,” Massad Boulos kisha alizungumzia wakati wa ziara yake mjini Kigali mazungumzo kati ya serikali ya Kongo na AFC-M23 huko Doha, nchini Qatar.
Tangu kutangazwa kwa kuanza kwa shughuli kwenye amana hiyo ya Kongo, ambayo inawakilisha 6% ya uzalishaji wa bati duniani, bei ya chuma imeshuka kwa 8%.