Mashariki mwa DRC: Shinikizo la Ulaya laongezeka dhidi ya Rwanda

Mawaziri 27 wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamekutana mjini Brussels siku ya Jumatatu ambapo wameamua kulegeza vikwazo vyao dhidi ya Syria. Kwa upande mwingine, wameamua kuiwekea Urusi awamu ya kumi na sita ya vikwazo na zaidi ya yote, kwa mara ya kwanza tangu Goma kuwa mikononi mwa M23, hatimaye waliweza kuchukua uamuzi wa pamoja kuhusu suala la jukumu la kijeshi la Rwanda katika kuunga mkono wanamgambo wa waasi wa M23 nchini DRC.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Brussels, Pierre Benazet

Ni Kaja Kallas, mkuu wa diplomasia ya Ulaya, ambaye ametangaza kwamba nchi 27 wanachama wa EU wameamua kusitisha mazungumzo ya kisiasa na Rwanda kuhusu masuala ya usalama na ulinzi. Haya ni matokeo ya kwanza yanayoonekana ya kulaaniwa kwa hatua ya jeshi la Rwanda katika miko miwili ya Kivu. Hadi sasa, Umoja wa Ulaya ulikuwa umelaani rasmi mashambulizi dhidi ya uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na uadilifu wa eneo lake, kisha kitengo cha Mambo ya Nje cha Umoja wa Ulaya kikamwita balozi wa Rwanda mjini Brussels siku ya Ijumaa. Kusimamishwa huku ni ishara kali ya kisiasa na nchi za Umoja wa Ulaya zinabainisha kwamba ni hatua ya kwanza.

Hali ni mbaya sana na tuko ukingoni mwa mzozo wa kikanda. Uadilifu wa eneo hauwezi kujadiliwa ama Kongo au Ukraine. Mkataba wa Umoja wa Mataifa unatumika sawa kila mahali. Kwa hivyo tunaunga mkono kwa uwazi mchakato wa amani wa Luanda na Nairobi ili kupata matokeo kupitia njia za kidiplomasia. Lakini pia tunachukua hatua kadhaa. Kwanza, mashauriano ya ulinzi wa Umoja wa Ulaya na Rwanda yamesitishwa. Pia kuna uamuzi wa kisiasa wa kutekeleza vikwazo kulingana na hali ilivyo. Tumeitaka Rwanda kuondoa wanajeshi wake na mkataba wa makubaliano wa malighafi muhimu utapitiwa upya.

Ubelgiji ilikuwa ya kwanza kutoa wito wa ushirikiano na programu zote za usaidizi kati ya EU na Rwanda kupunguzwa, msimamo ambao sasa umeidhinishwa na Ufaransa, ambayo ilishiriki kikamilifu katika kuandaa orodha sahihi zaidi ya vikwazo. Orodha ambayo inajumuisha taasisi ambayo mali zake barani Ulaya zimezuiliwa na maafisa tisa wa Rwanda ambao pia wamepigwa marufuku kuingia nchi za EU.

Ilikuwa ni hatua ya pili ya msururu wa vikwazo dhidi ya Rwanda, lakini kupitishwa kwake kulizuiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Luxembourg Xavier Bettel. Aliwataka wenzake kusubiri kuanzisha vikwazo hivyo, kusubiri matokeo ya mkutano wa pamoja wa mawaziri wa Februari 28 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mgogoro wa kidiplomasia kwa Kigali

Umoja wa Ulaya utatumia vikwazo vya hali ya juu, kile unachokiita “hatua za vikwazo” kwa mtu binafsi: kuzuia mali katika Ulaya na kupiga marufuku kukaa katika eneo la umoja huo. Itakumbukwa tu kwamba, vikwazo vya Marekani tayari vinamlenga Jenerali James Kabarebe, Waziri wa zamani wa Ulinzi na mshauri wa rais wa Rwanda.

Kigali inasema vikwazo hivi vya Ulaya ni kikwazo kikubwa cha kidiplomasia, kwa sababu vinaashiria makubaliano ya nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya ya kuishutumu kwa kuingilia kati uhuru na uadilifu wa eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita, Umoja wa Ulaya uliitaka Rwanda kuondoa wanajeshi wake katika miko miwili ya Kivu na kusitisha uungaji wake mkono kwa M23. Kwa hivyo vikwazo hivi ni hatua ya kwanza iliyokusudiwa kuitenga Kigali kutokana na hali mashariki mwa DRC. Lakini EU, ambayo inachukulia vikwazo vya Marekani kuwa vikali sana, inataka kuweka baadhi ya hatua ili kudumisha shinikizo kwa Rwanda.

EU pia inatishia kusitisha ushirikiano na Rwanda kuhusu malighafi muhimu na madini adimu.