Mashariki mwa DRC: Operesheni ya pamoja na jeshi la Uganda yaendelea kutanuka kuelekea Bunia

Kaskazini-mashariki mwa DRC, vikosi vya Uganda vinaimarisha uwepo wao. Wametumwa kwa miaka kadhaa kama sehemu ya makubaliano kati ya nchi hizo mbili. Operesheni ya pamoja na jeshi la Kongo kuwasaka waasi wa ADF, haswa katika mkoa wa Kivu Kaskazini na sasa huko Ituri.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi

Tangazo la jeshi la Uganda linaenda sambamba na kusonga mbele kwa waasi wa M23 wakungwa mkono na wanajeshi wa Rwanda kuelekea kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kaskazini. Lakini kwa mamlaka ya Kongo, ni suala la kuratibu vyema upanuzi wa shughuli za pamoja.

Kwa siku kadhaa, majeshi hayo mawili yamekuwa yakifanya kazi ya “kuoanisha” matendo yao ndani ya mfumo wa Operesheni Shujaa. Operesheni hii ya pamoja ilizinduliwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita na ilikuwa na dhamira yake kuu ya kupigana na kundi la ADF, ambalo ni hatari sana katika mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini.

Upanuzi wa ujumbe wa pamoja

Maafisa wa kijeshi walikutana kwa mara ya kwanza siku ya Jumatatu, Februari 17, katika jiji la Boga. Majenerali wa Uganda kisha walielekea Bunia, mji mkuu wa mkoa kwa mikutano zaidi ya matayarisho siku ya Jumanne, wakati karibu wanajeshi mia moja wa jeshi la Uganda pia waliingia katika eneo hilo. Majadiliano hayo yanatarajiwa kuendelea angalau leo Jumatano.

Kulingana na chanzo cha kijeshi, pamoja na upatanishi huu, majadiliano yanapaswa kuzingatia upanuzi wa misheni ya pamoja kwa makundi mengine yenye silaha yaliyopo katika mkoa huo. Kiongozi wa mashirika ya kiraia anazungumzia uwezekano wa kutumwa wanajeshi katika eneo la Djugu, ambako makundi mawili ya wanamgambo, Codeco na Zaire, wanapigana katika mzozo ambao ni hatari sana kwa raia.