Mashariki mwa DRC: Kinshasa na AFC/M23 bado wanavutana katika mazungumzo ya amani

Wakati tahadhari ya kimataifa ikielekezwa kwa Marekani, ambayo imepokea rasimu ya awali ya makubaliano ya amani ya mashariki mwa DRC kutoka Kigali na Kinshasa, kivutio pia kiko Doha, ambapo wajumbe kutoka serikali ya Kongo na vuguvugu la waasi la AFC/M23 wanakutana kwa mara ya tatu.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa serikali ya Kongo na vuguvugu la waasi la AFC/M23 waliwasili mjini Doha mwishoni mwa wiki iliyopita, bila mabadiliko ya dhahiri katika muundo wao: bado kimsingi wanaundwa na mafundi waliobobea katika nyanja za usalama na ujasusi. Kazi ilianza tena Jumapili, Mei 4, lakini bila mawasiliano yoyote ya moja kwa moja mwanzoni. Kila upande kwanza ulifanya kazi kivyake kabla ya kuletwa pamoja kwenye meza ya majadiliano.

Pande zote mbili zinadai kutaka “kufanya kazi kuelekea kuhitimisha makubaliano ambayo yataruhusu kuanzishwa kwa usitishaji vita unaofaa,” lakini kwa ukweli, hali inabaki kuwa ya wasiwasi na bado kuna mashaka ya kufikia suluhu ya kudumu. Tangu tamko lao la pamoja siku kumi zilizopita, hakuna maendeleo madhubuti yaliyopatikana. Kinyume chake, vizuizi vinaendelea, mapigano yameanza tena. AFC/M23 inasonga mbele kaskazini mwa Ziwa Edward na imechukua udhibiti wa Lunyasenge, katika eneo la Lubero. Harakati nyingine za askari pia zimeripotiwa karibu na Kashebere, katika eneo la Walikale.

Kutokana na kuzorota huku, wapatanishi wanasisitiza kudumisha mazungumzo ya wazi. Doha imefufua tena mazungumzo, kwa kuhusisha Marekani, ambayo ilichukua jukumu kuu katika kuanza tena kwa majadiliano. Chini ya shinikizo hili, wajumbe walihimizwa kurejea kwenye meza ya mazungumzo, kwa mchakato ambao muda wake, katika hatua hii, haujajulikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *