Mashariki mwa DRC: HRW ina wasiwasi kuhusu shinikizo kwa wanaharakati na waandishi wa habari

Shirika la kimataifa la Haki za Bindamu la Human Rights Watch (HRW) lina wasiwasi kuhusu kupungua kwa nafasi ya raia katika maeneo yanayodhibitiwa na M23.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliyotolewa siku ya Jumanne, Machi 11, shirika hili lisilo la kiserikali la haki za binadamu linadai kwamba waasi wa M23, wakiungwa mkono na Rwanda, wametoa shinikizo nyingi na kuwakamata wanaharakati wa mashirika ya kiraia na waandishi wa habari, hata kufikia kuwaua baadhi yao. Mbinu ambayo tayari inatumika katika maeneo yanayokaliwa na M23 na ambayo sasa inaenea katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, wakati mwingine kwa msaada wa Rwanda.

Mbinu ambayo tayari inatumika katika maeneo yanayokaliwa na M23 na ambayo sasa inaenea katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, wakati mwingine kwa msaada wa Rwanda.

Ripoti ya Human Rights Watch (HRW) inabainisha kuwa “M23 ina historia ndefu ya kutumia vitisho kuzuia upatikanaji wa habari kwa watu na kuzima sauti za wakosoaji.” Na tangu kutekwa kwa Goma mwishoni mwa mwezi wa Januari, kisha Bukavu mwezi Februari, shinikizo kwa wanaharakati, waandishi wa habari na wale wanaokataa kufuata sheria zao imeongezeka. Wale waliojaribu kutoroka kupitia Rwanda hawakufikia ndoto yao, anasema Clémentine de Montjoye, mtafiti wa Human Rights Watch katika kanda ya Afrika:

“Katika kesi kadhaa za watu kuzuiliwa tulizoandika, tumebaini kuwa watu kadhaa walipigwa. Kwa upande wa mtu ambaye alikamatwa na mamlaka ya Rwanda kukabidhiwa M23, msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka alituthibitishia kuwa M23 waliomba mtu huyu azuiliwe na kisha kutymwa kwao, na hii kwa kazi yake juu ya mzozo ambao waliuona kuwa ni dhidi ya M23. “

Wakati huo huo mwanaharakati anashuhudia kwamba maisha yake pia yako hatarini kwa sababu ya huduma ya matibabu aliotoa kwa wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa vita vya Goma mwishoni mwa mwezi wa Januari. “Nimetoroka majaribio kadhaa ya mauaji ya watu wenye silaha wasiojulikana,” anasema kijana mtu huyo, ambaye tangu wakati huo amekimbia mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini. “Ninahofia familia yangu iliyosalia Kongo,” anasema kiongozi wa mashirika ya kiraia ambaye pia amekimbilia nje ya nchi. “Mke wangu anapokea jumbe kutoka kwa watu wakimuuliza yuko wapi, wakimwambia watamkamata, yote hayo kwa kulipiza kisasi dhidi yangu,” anaongeza.

Kilele cha dhuluma hizi ni kifo, chini ya mazingira yasiyoeleweka, cha mwimbaji Delcat Idengo mnamo Februari 13 huko Goma, na mwanaharakati wa Lucha Pierre Katema Byamungu mnamo Februari 12 katika eneo la Kalehe, Kivu Kusini. Siku moja baada ya kifo chake, shirika la kiraia liliripoti kwamba kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 aliuawa pamoja na wanaharakati wengine wanne, baada ya “kukamatwa na kulazimishwa kusafirisha vifaa vya waasi.” Madai haya yalikataliwa moja kwa moja na waasi, ambao, katika ujumbe wa Twitter, walikanusha kuwakamata au kuwatendea vibaya waandishi wa habari na wanaharakati, na kulaani “matumizi mabaya ya ushawishi kuharibu sifa ya kundi lao.”

Clémentine de Montjoye anasema, hata hivyo, kwamba kabla ya M23 kufika katika miji hii, hali ilikuwa si shwari kabisa, hasa kwa waandishi wa habari. “Wengi wao walikabiliwa na shinikizo na vitisho kutoka kwa mamlaka ya Kongo ambayoi kudhibiti jinsi walnavyoshughulikia mzozo,” amesema. Ripoti hiyo pia inabainisha kuwa upatikanaji wa maeneo yanayokaliwa na M23 sasa unaendana na kibali na unafanywa kwa usaidizi wa maafisa wakuu wa Rwanda, wakiwemo wajumbe wa msemaji wa serikali ya Rwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *