
Hospitali katika miji kadhaa ya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini zinakabiliwa na uhaba wa damu, wakati kukiripotiwa mapigano kati ya jeshi la Kongo na washirika wake kwa upande mmoja na AFC/M23 inayoungwa mkono na Rwanda kwa upande mwingine.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi
Kutokana na mapigano kati ya FARDC na washirika wake dhidi ya AFC/M23 inayoungwa mkono na Rwanda, hospitali kadhaa katika miji ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini zinakabiliwa na uhaba wa damu, ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuwatibu waliojeruhiwa kwa risasi au milipuko.
Ili kurekebisha hili, serikali ya Kongo ilizindua kampeni ya kukusanya damu mjini Kinshasa mwanzoni mwa mwezi wa Februari. Shehena ya kwanza ilitumwa Machi 4 hadi Goma na Bukavu lakini ilikabiliwa na matatizo mengi.
Kwanza, madereva kadhaa walikataa kusafirisha mifuko hii kwa sababu ya hali inayojiri katika mikoa hiyo. Kisha, vikwazo vya utawala vilifanya uwasilishaji kuwa mgumu. Wakati kundi la kwanza la vifaa vya matibabu na dawa lilipotumwa siku 13 zilizopita, kila kitu kilikuwa kimeidhinishwa kutoka Brussels hadi Goma, isipokuwa damu, kulingana na vyanzo kadhaa vilivyowasiliana na RFI.
Safari hiyo ilihitaji kupita Brussels, Nairobi, Kigali, kisha Rubavu, nchini Rwanda, kabla ya kufika Goma na Bukavu. Safari ndefu na ya gharama kubwa, hasa kwa vile mifuko hii ya damu ya mililita 500 kila moja lazima iwekwe kwenye halijoto maalum ili kuepuka kuharibika. Shirika la Afya Duniani (WHO) liliwezesha operesheni hiyo kwa kupata ukanda salama, hivyo kuruhusu utoaji wa kundi la kwanza.
Zoezi la pili la kusafirisha fifaa hivyo limepangwa lakini kwa changamoto sawa za vifaa. Wakati kampeni hiyo ilipozinduliwa, Waziri wa Afya aliweka lengo la mifuko ya damu 5,000 iliyokusanywa. Idadi iliyofikiwa na hata kuzidi, anahakikisha, akibainisha kuwa mifuko 1,200 tayari imetumwa mashariki mwa nchi. Lakini shida nyingine hutokea vifaa hivyo vinapowasili: uhifadhi wa damu na usambazaji wake kwa hospitali. Baadhi ya vituo vya afya vimeharibiwa na vurugu hizo na hivyo kufanya huduma kwa wagonjwa kuwa ngumu.