Mashariki mwa DRC: Baraza la Amani na Usalama la AU lakutana

Mzozo wa mashariki mwa DRC umekuwa kiini cha mkutano wa Baraza la Amani na Usalama (PSC) la Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea hivi sasa kabla ya mkutano wa mwaka wa wakuu wa nchi.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Migogoro miwili ilikuwa kwenye ajenda ya baraza hili, vita vya Sudani na mashariki mwa DRC. Lakini katika hotuba yake ya ufunguzi, Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa tume ya AU, ameitaja tu Sudani, anaripoti mwandishi wetu maalum mjini Addis Ababa, Florence Morice. Hakuna neno lolote kuhusu DRC, ishara bila shaka ya mvutano unaotawala, ingawa AFC-M23 imepata mafanikio mapya katika mkoa wa Kivu Kusini.

Kwa kukosekana kwa Félix Tshisekedi, hakukuwa na mkutano wa ana kwa ana na Paul Kagame, lakini mazungumzo yalikuwa ya kusisimua. “yalikuwa na mvutano,” mshiriki mmoja amesema. Kama ishara ya mvutano huu, mkutano na waandishi wa habari ambao ulipangwa baada ya kikao hicho ulifutwa usiku.

Viongozi kadhaa wa nchi pia waliondoka kwenye mkutano muda mfupi kabla ya kumalizika, akiwemo Rais Kagame na mpatanishi katika mzozo wa DRC, rais wa Angola Joao Lourenço

Kauli ambayo inapaswa kuendana na mkutano mkuu wa Dar es Salaam

Miongoni mwa masuala yenye utata: lile la wanajeshi wa Rwanda waliopo katika ardhi ya Kongo. DRC kwa mara nyingine tena imetoa wito kwa Kigali kutengwa na kushtumiwa kwa jukumu lake katika mzozo huu. Nchi kadhaa za kusini mwa Afrika zimeunga mkono maoni haya, ikiwa ni pamoja na Zimbabwe, lakini bila mafanikio.

Tamko la mwisho kwa hiyo linapaswa kuendana na hitimisho la mkutano wa kilele wa Dar es Salaam, bila kwenda mbali zaidi: wito wa kusitishwa kwa mapigano, kuheshimu uhuru wa eneo la DRC, kuanza upya kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande zote, ikiwa ni pamoja na kati ya M23 na Kinshasa, na kuunganishwa kwa mchakato wa Luanda na Nairobi.

Baada ya mkutano huo, Moussa Faki Mahamat ametoa wito kwa mataifa ya Afrika kuhamasishana kutatua mgogoro huo, kulingana na mwandishi wetu wa habari mjini Addis Ababa, Clothilde Hazard: “Kwetu sisi, usitishaji vita lazima uzingatiwe kama ilivyoamuliwa na jumuiya mbili za kiuchumi za kikanda. Na ninaamini kwamba hii imethibitishwa tena leo kwenye Baraza la Amani na Usalama, lazima kabisa tuelekee kile kilichokubaliwa, yaani kuelekea mazungumzo ya utatuzi wa mzozo huu. “

“Uhamasishaji lazima uimarishwe kwa ajili ya misaada na usaidizi wa kibinadamu kwa mamilioni ya watu walio katika dhiki nchini Sudani” , 

Moussa Faki Mahamat pia amesema kuhusu hali nchini Sudani.