
Mashabiki wa soka waliohudhuria mechi ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya mjini Paris kati ya Ufaransa na utawala wa Kizayuni wa Israel walipiga filimbi na kuzomea wakati wimbo wa taifa wa utawala huo ulipopigwa mwanzoni mwa mchezo huo.
Mechi ya jana Alhamisi ilichezwa mbele ya umati mdogo wa watu na ulinzi mkali ikiwa ni wiki moja baada ya vurugu huko Amsterdam kati ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina na mashabiki wa Israel wenye chuki na Palestina na muuqawama.
Mashabiki wanaounga mkono Palestina walipiga miluzi, filimbi na makele kuzuia wimbo wa taifa wa utawala wa Kizayuni usisikike kama ishara ya kuonyesha upinzani wao kwa jinai zinazofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina.
Rais Emmanuel Macron, ambaye alihudhuria mechi hiyo na Waziri Mkuu Michel Barnier ambapo matokeo yaliikuwa sare ya bila kufungana, alisema hapo kabla kwamba eti Ufaransa haitakubali chuki dhidi ya Wayahudi.
Wiki iliyopita kulienea video mtandaoni zinazowaonyesha wanaojiita mashabiki wa soka wa Israel wakirarua bendera za Palestina zilizokuwa zimepeperushwa katika nyumba za wakazi.
Waungaji mkono wa Palestina waliamua kukabiliana na mashabiki hao wenye chuki wa timu ya soka ya Maccabi ya Israel.
Timu ya soka ya Maccabi Tel Aviv ilimenyana na timu ya Ajax Amsterdam, ambapo ilichapwa 5-0 na timu hiyo ya Uholanzi katika uwanja wa nyumbani wa Ajax.