
Mashabiki wa mpira wa Kizayuni waliokuwa wakitizama mechi ya soka katika mji wa Amsterdam nchini Uholanzi wameshambuliwa na kuchezea kipigo baada ya kuivunjia heshima bendera ya Palestina.
Kanali ya Sahab imelinukuu shirika la habari la IRNA na kuripoti kuwa, mashabiki wa soka wa Kizayuni nchini Uholanzi wameichana bendera ya Palestina baada ya kumalizika mechi kati ya timu za Maccabi ya Tel Aviv na Ajax ya Amsterdam.
Vijana wa Kiislamu waliokuwa na hasira waliwashambulia watazamaji wa Kizayuni na kuwapiga baada ya kuichana bendera ya Palestina.
Wazayuni watano wamejeruhiwa katika vurugu hizo. Ofisi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu imetangaza kuwa ndege mbili zimetumwa Uholanzi ili kuwarejesha watazamaji hao wa Kizayuni.