Marekani yasitisha kupeana taarifa za intelijensia na Ukraine

Marekani “imesitisha” ushirikiano wa kijasusi na Ukraine, mkuu wa CIA John Ratcliffe amesema siku ya Jumatano. Hata hivyo, mazungumzo kati ya Kyiv na Washington yanatarajiwa kuanza tena hivi karibuni. Mkuu wa ofisi ya rais ya Ukraine Andriy Yermak alikutana kwa mazungumzo na mshauri wa usalama wa taifa wa Donald Trump Mike Waltz siku ya Jumatano. Mkutano unaweza kufanyika katika siku za usoni.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Kyiv iko chini ya shinikizo la Marekani. Ukraine imesema siku ya Jumatano, Machi 5, kwamba inafanyia kazi mazungumzo mapya na Marekani baada ya Washington kutangaza kuwa “inasitisha” kupeana taarifa za intelijensia na Ukraine, kufuatia kusitishwa kwa msaada wake wa kijeshi, mambo mawili muhimu katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Kyiv inaendelea kukabiliana na mkanganyiko kufuatia mkutano wa siku ya Ijumaa katika Ikulu ya White House kati ya Rais Volodymyr Zelensky na Donald Trump, wakati ambapo Washington imeanza tena mazungumzo ya moja kwa moja na Moscow, na kuzua hofu ya kutelekezwa kwa Ukraine.

Tangu wakati huo, Volodymyr Zelensky amefanya ishara nyingi za kutuliza mgogoro a Maekani, huku akiendelea na mazungumzo na nchi za Ulaya, ambazo zimetakiwa kutoa msaada muhimu wa Marekani ikiwa mgogoro hautatatuliwa.

Mkutano katika siku za usoni

Katika muktadha huu, mkuu wa ofisi ya rais wa Ukraine Andrii Yermak amezungumza kwa njia ya simu siku ya Jumatano na mshauri wa usalama wa taifa wa Donald Trump Mike Waltz.

Waawili hao “walijadili hatua zaidi za kuchukuliwa ili kufikia amani ya haki na ya kudumu” nchini Ukraine. Walikubaliana kwamba timu zao zitakutana katika siku za usoni “ili kuendeleza kazi hii muhimu,” Andriy Yermak amesema kwenye Telegram.

“Timu za Ukraine na Marekani zimeanza kufanyia kazi mkutano ujao,” ameongeza Rais Zelensky, akisema anatumai “kuona matokeo ya kwanza wiki ijayo.”

Kiongozi huyo wa Ukraine anatazamiwa kuhudhuria mkutano maalum wa kilele wa Umoja wa Ulaya wenye wanachama 27 mjini Brussels siku ya Alhamisi, huku Wazungu wakitafuta kuelezea jibu la pamoja kuhusu maelewano kati ya Washington na Moscow na kuihakikishia Ukraine. Hata hivyo, hakuna msaada mpya wa kijeshi unaotarajiwa katika mkutano huu usio wa kawaida.

Licha ya matatizo hayo, Volodymyr Zelensky alisema Jumatano kwamba amani ya kudumu nchini Ukraine “inawezekana kabisa” ikiwa Ulaya itafanya kazi kwa pamoja na Marekani.

Mkuu wa nchi ya Ukraine anadai kudhaminiwa kwa nguvu za kiusalama kutoka kwa washirika wake wa nchi za Magharibi katika muktadha wa mazungumzo yanayowezekana ili kuhakikisha kuwa jeshi la Urusi halivamii tena nchi yake baada ya kusitisha mapigano kwa dhahania.