
Mshauri wa rais wa Marekani, Donald Trump kuhusu masuala ya Afrika, Massad Boulos, Alhamis ameripoti kufanya mazungumzo na rais wa Rwanda, Paul Kagame na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi, kuhusu rasimu ya mkataba wa amani wakati huu Washington ikijaribu kuzipatanisha pande hizo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Marekani kwa sasa inaendelea kusubiri majibu ya mwisho yanayotarajiwa kuwasilishwa wikendi hii kutoka Kinshasa na Kigali, kuhusu makubaliano ya kuelekea kupata amani ya kudumu.
Kulinagana na Massad licha ya kwamba Marekani ina matarajio makubwa kutoka kwa Kigali na Kinshasa, amekiri huenda mapendekezo yatakayowasilishwa yatahitaji kufanyiwa maboresho.
Kwa sasa Marekani inasema imeridhishwa na hatua zilizopigwa katika mazungumzo kati ya rais Paul Kagame na Felix Tshisekedi.
DRC na Rwanda mapema mwezi huu ziliwasilisha rasimu ya mapendekezo yao kuhusu namna amani inaweza kupatikana mashariki mwa nchi hiyo.
Baada ya kila kitu kukamilika, Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka mataifa ya Rwanda na DRC wataalikwa tena jijini Washington.