
Baraza la Usalama la Taifa la Marekani limeeleza tu wasiwasi na masikitiko yake kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya mahema ya wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
Baraza la Usalama la Taifa la Marekani limesema leo Jumanne asubuhi kwamba, limejibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu kuchomwa mahema ya wakimbizi wa Kipalestina katika Hospitali ya Al-Aqsa, na kwamba picha za raia waliokimbia makazi yao wakiungua katika shambulio la anga la utawala Israel huko Gaza ni la kusikitisha sana.
Baraza hilo limedai kuwa, “kilichotokea ni cha kutisha, ingawa Hamas wamekuwa wakijaribu kutumia raia kama ngao za binadamu karibu na Hospitali ya Al-Aqsa.
Utawala wa Kizayuni umeteketeza kwa moto mahema zaidi ya 30 ya Wapalestina waliokimbia makazi yao waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya al-Aqsa huko Gaza na kuua na kujeruhi makumi ya wengine.
Radiamali dhaifu ya serikali ya Marekani dhidi ya mauaji ya kimbari ya utawala ghasibu wa Israel yameufanya utawala huo haramu kuendeleza jinai zake za kinyama huko Palestina na Lebanon kwa uungaji mkono wa kisheria na kijeshi wa Marekani na waitifaki wake wa Magharibi.
Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kwamba, idadi ya mashahidi huko Gaza tangu tarehe 7 Oktoba 2023, tangu oparesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, imefikia watu 42,289 na waliojeruhiwa imefikia 98,684.