Wanadiplomasia wa Marekani, wameonesha imani kuwa mapendekezo ya usitishaji mapigano kati ya Urusi na Ukraine yatakubaliwa katika wiki chache zijazo, wakati huu rais Donald Trump na mwenzake wa Urusi, Vladmir Putin wakitarajiwa kuzungumza wiki hii.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Haya yanajiri wakati huu mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili wakijadili mpango huo.
Juma hili Marekani ilipendekeza kusitishwa kwa mapigano katika vita iliyodulu kwa zaidi ya miaka mitatu baada ya mazungumzo ya nchini Saudi Arabia, ambayo Kyiv ilikubali.
Hata hivyo licha ya kupokea mpango huo toka kwa Marekani, Rais wa Urusi Vladimir Putin hajatoa jibu la wazi, badala yake ameorodhesha mlolongo wa masharti na kuibua “maswali” kuhusu pendekezo hilo.

Rais wa Ukraikne, Volodymyr Zelensky, hapo jana aliishutumu Kremlin kwa kutotaka kusitisha vita na kuonya kwamba Moscow inataka kwanza “kuboresha hali yao katika uwanja wa vita” kabla ya kukubaliana na usitishaji wowote wa mapigano.
Moscow inasema waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, alimpigia simu mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov na kujadiliana masuala kadhaa kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Washington.