Marekani imejiondoa rasmi katika mkataba mkubwa wa hali ya hewa, mpango wa mabilioni ya dola uliozinduliwa mwaka wa 2021 ili kusaidia mataifa yanayoibukia kiuchumi kuondokana na nishati ya makaa ya mawe na vyanzo vingine vya nishati ambazo sio jadidifu.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Licha ya Washington kujiondoa, washirika wengine, ikiwemo Ufaransa, Ujerumani, Umoja wa Ulaya, Uingereza, Uholanzi na Denmark, wamesalia kujitolea kutekelezwa kwa mpango huo.
Aidha wataalamu wanasema kuondoka kwa Marekani kwenye mpango huo kutaziathiri pakubwa Afrika Kusini na Indonesia, ambazo ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa mkataba huo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, miradi ya ruzuku ambayo hapo awali ilifadhiliwa na taifa hilo ikiwemo katika awamu wa upangaji na utekelezaji, imefutwa.
Chini ya makubaliano na Afrika Kusini, nchi hiyo iliahidiwa ruzuku ya dola milioni 56 na dola bilioni 1 za ziada katika uwekezaji unaowezekana wa kibiashara.