Marekani yabatilisha viza zote zilizotolewa kwa raia wa Sudan Kusini

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema Washington inabatilisha viza zote zilizotolewa kwa raia wote wenye pasi za kusafiria za Sudan Kusini, akiutuhumu utawala wa Juba kwa kukataa kuwapokea raia wake waliofukuzwa nchini humo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake Rubio amesema kila nchi lazima ikubali kuwapokea raia Wake wanaorudishwa nyumbani katika muda unaokubalika ikiwemo wale waliofukuzwa na Washington.

Rubio ameongeza kuwa kufuatia hatua ya utawala wa mpito wa Juba kushindwa kutimiza wajibu Wake kwa wakati, Serikali yake imeamua kufuta viza zilizotolewa kwa raia Wake wanaopeza hifadhi maalumu nchini humo.

Aidha waziri Rubio amesema nchik yake itazuia utolewaji wa vibali vya kuingia nchini humo kwa raia wengine wa Sudan Kusini.

Hii ni mara ya Kwanza kwa utawala wa Trump, kufuta viza kwa raia wenye pasi halali za kusafirikia toka taifa jingine, ikiwa ni muendelezo wa sera yake ya kufukuza wale anaosema wageni wasio na vibali nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *