Marekani: Waziri wa Ulinzi ahusishwa katika uvunjaji mwingine wa usalama

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth, ambaye alihusishwa na uvunjaji wa usalama mwezi uliopita, pia ametoa taarifa kuhusu shambulio la kundi jingine la Signal nchini Yemen, vyombo kadhaa vya habari vya Marekani viliripoti Jumapili.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Bw. Hegseth, mtangazaji wa zamani wa Fox News, ndiye anayehusika na uchunguzi wa ndani wa Pentagon baada ya kushiriki habari nyeti kuhusu huduma ya ujumbe wa Signal mnamo Machi 15 katika mazungumzo ambayo yalijumuisha mwandishi wa habari ambaye inaonekana alialikwa kimakosa.

Kulingana na Gazeti la New York Times na CNN, Bwana Hegseth pia alishiriki katika mazungumzo kwenye kundi jingine la Signal siku hiyo, ambayo yalihudhuriwa na mkewe, kaka yake, mwanasheria wake, “pamoja na watu wapatao kumi kutoka kwa wasaidizi wake wa kibinafsi na wa wake wa kazini.”

Gazeti kuu la kila siku la New York, ambalo linataja “watu wanne wanaofahamu mazungumzo haya,” linabainisha kuwa Waziri wa Ulinzi alitangaza katika hafla hii ratiba sahihi za safari za ndege ambayo ililenga waasi wa Houthi nchini Yemen, “kimsingi mipango ya mashambulizi sawa na yale aliyokuwa ameshiriki siku hiyo kwenye kundi jingine la Signal.”

Gazeti hilo limesema mke wa waziri, mwandishi wa habari na pia mfanyakazi wa zamani wa Fox News, hajaajiriwa na Pentagon, wakati kaka na wakili wa Bw. Hegseth wanashikilia nyadhifa mbalimbali.

“Lakini ni vigumu kuona ni kwa nini yeyote kati yao angehitaji kujua kuhusu mashambulizi ya karibu dhidi ya Wahouthi nchini Yemen,” Gazeti la NYT inaandika.

Kulingana na gazeti hilo, maafisa wa Pentagon walikuwa wamemuonya waziri huyo siku chache mapema kwamba hapaswi kujadili habari kuhusu mashambulizi nchini Yemen kwenye Signal, huduma ya utumaji ujumbe iinayoonekana kuwa salama kuliko njia rasmi ambazo kawaida hutumika kwa data nyeti.

Akijibu ripoti hizo, msemaji wa Pentagon Sean Parnell ameshutumu Gazeti la New York Times kuwa “chanzo cha kumchukia Trump.”

“Hakukuwa na taarifa za siri katika mijadala yoyote kuhusu Signal, bila kujali jinsi wanavyojaribu kuzungusha hali ya mambo,” amesema, bila kutoa maelezo zaidi.

Pia siku ya Jumapili, msemaji wa zamani wa Bw. Hegseth kwa Pentagon, John Ullyot, alichapisha nakala ya maoni ya vitriolic inayoelezea “mwezi wa machafuko kamili katika Pentagon.”

“Rais Donald Trump ana historia ya kuwawajibisha maafisa wake wakuu. Kutokana na hili, ni vigumu kuona Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth akisalia katika nafasi yake kwa muda mrefu zaidi,” Ullyot ameandika.

Chama cha upinzai cha Democratic kimechukua hatua haraka. Mjumbe wa Kamati ya Seneti ya vikosi vya jeshi Jack Reed amemtaka mkaguzi mkuu wa Pentagon kujumuisha madai ya hivi punde katika uchunguzi wake.

“Ikiwa tukio hili litathibitishwa, ni mfano mwingine wa kusikitisha wa waziri Hegseth wa kutozingatia sheria na itifaki ambazo wanajeshi wengine wote wanatakiwa kufuata,”mekatika taarifa yake.

Wakati wa kashfa ya kwanza ya “Signalgate”, Rais Donald Trump aliwatetea mawaziri wake waliohusika katika mazungumzo na mwandishi wa habari Jeffrey Goldberg wa jarida la The Atlantic.

Mike Waltz, mshauri wake wa usalama wa kitaifa, alichukua “kuwajibika” kwa hilo, akielezea kwamba alikuwa ameunda kikundi kwenye Signal.

Kulingana na Gazeti la NYT, kundi lingine liliundwa na Bw. Hegseth mwenyewe kabla ya kuchukua mamlaka kama waziri.

Maafisa watatu wakuu wa Pentagon pia walifutwa kazi wiki iliyopita kufuatia uvujaji usiojulikana.

Maafisa waliohusika – Naibu MkurugenziDarin Selnick na washauri Dan Caldwell na Colin Carroll – walijibu Jumapili kwa kutoa taarifa wakishutumu Wizara ya Ulinzi kwa “kuwachafua kwa mashambulizi yasiyo na msingi.”

“Kwa wakati huu, bado hatujaambiwa ni sababu gani mahususi tunazochunguzwa, ikiwa uchunguzi unaendelea, au hata kumekuwa na uchunguzi wa uvujaji huo,” wameandika kwenye mitandao ya kijamii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *