
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza Jumapili, Juni 8, kwamba askari wa kikosi cha walinzi wa taifa aliowatuma Los Angeles kinyume na matakwa ya mamlaka ya jimbo hilo kushughulikia maandamano dhidi ya sera yake ya uhamiaji watarejesha “utulivu.”
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kutumwa kwao kunakuja katika siku ya tatu ya maandamano yaliyokumbwa na makabilianono na vurugu katika jiji kuu la California, ambako wanaishi watu wengi kutoka jamii kubwa ya Wahispania, wakati wakaazi walijaribu kupinga kukamatwa kwa wahamiaji kwa nguvu kulikofanywa na mamlaka ya Uhamiaji ya Shirikisho (ICE).
“Mna watu wenye jeuri wanaochochea vurugu, na hatutawaacha waondoke,” amewaambia waandishi wa habari. “Tutarejesha utulivu,” ameahidi, pia akisema anafikiria kutuma wanajeshi mahali pengine. “Hatutaruhusu jambo la aina hii kutokea kwa nchi yetu.”
“Tutarejesha utulivu,” ameongeza rais huyo kutoka chma cha Republican, akisema amekuwa akifuatilia hali hiyo “kwa karibu sana.” Ameongeza kuwa hajasita kutuma wanajeshi kwingineko nchini Marekani ikibidi. “Hatutaruhusu jambo la aina hii kutokea kwa nchi yetu,” amesema. “Tukiona hatari kwa nchi yetu na raia wetu, tutakuwa thabiti sana katika kutekeleza sheria na kudumisha utulivu,” amebainisha.
“Matumizi mabaya ya kutisha ya madaraka,” amelaani magavana wa California kutoka chama cha Democratic
Kulingana na Kenneth Roth, mkuu wa zamani wa shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch, hii itakuwa mara ya kwanza tangu mwaka 1965 kwa rais kupeleka wanajeshi hao bila ombi la awali kutoka kwa gavana wa jimbo.
Magavana wa chama cha Democratic nchini Marekani wameshutumu “utumiaji mbaya wa madaraka” uliofanywa na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alituma wanajeshi 2,000 wa kikosi cha walinzi wa taifa huko Los Angeles, kinyume na matakwa ya Gavana wa California kutoka chama cha Democratic, Gavin Newsom. “Uamuzi wa rais Trump kupeleka wanajeshi wa kikosi cha walinzi wa taifa huko California ni matumizi mabaya ya kutisha ya madaraka,” magavana walisema katika taarifa ya pamoja. “Ni muhimu tuheshimu mamlaka kuu ya magavana wa taifa letu kusimamia wanajeshi wa kikosi cha walinzi wao wa taifa,” wameongeza, wakisisitiza uungwaji mkono wao kwa Gavin Newsom.
Gavana wa California alipinga hatua hiyo, akiiita “uchochezi wa kimakusudi” na kudai kwamba “itaongeza tu mivutano.” “Nilimpigia simu hivi majuzi usiku. Nikasema, ‘angalia, unapaswa kulishughulikia hili. Vinginevyo, ninatuma askari.’ Na ndivyo tulivyofanya,” rais Donald Trump amesema Jumapili. Onyo ambalo amefuata tangu wakati huo.
Rais wa Mexico atoa wito kwa Washington kutowachukulia wahamiaji kama ‘wahalifu’
Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum ametoa wito kwa Marekani siku ya Jumapili, Juni 8, kutowachukulia wahamiaji kama wahalifu kufuatia shambulio huko Los Angeles ambapo, amebainisha, raia 35 wa Mexico walikamatwa.
“Wamexico wanaoishi Marekani ni (…) wanaume na wanawake wenye busara na waaminifu ambao walikwenda Marekani kutafuta maisha bora na kuhudumia familia zao. Wao si wahalifu,” amesema wakati wa hotuba kwa taifa.
Ajira ya wahamiaji “pia inasaidia uchumi wa Marekani,” amesisitiza.
Wanajeshi wa Marekani walianza kuwasili Los Angeles siku ya Jumapili kwa agizo la Donald Trump, kufuatia siku mbili za maandamano wakati mwingine yenye vurugu dhidi ya sera yake ya uhamiaji. “Hatukubaliani na mbinu hii ya kushughulikia hali ya uhamiaji, ambayo haihusishi mashambulizi au ghasia,” ametangaza, akitoa wito wa kuheshimiwa kwa haki za wahamiaji. Bi Sheinbaum amesema kuwa wanadiplomasia wa Mexico walikuwa wakiwasiliana na Wamexico 35 wanaozuiliwa nchini Marekani.