
Shauri jipya lililowasilishwa katika mahakama za Marekani, linaonesha kuwa maofisa wa idara ya uhamiaji nchini humo, wameanza kuwafurusha wahamiaji zaidi ya 12 kutoka Asia kwenda Sudan Kusini, kinyume cha sheria.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii imechukuliwa licha ya mahakama tarehe 7 ya mwezai huu kuzuia mpango mwengine wa kuwahamishia raia hao katika nchi za Libya na Saudi Arabia.
Mapema mwezi Aprili, utawala wa rais Trump ulifuta visa zilizokuwa zinashikiliwa na raia wa Sudan Kusini katika juhudi za Washington kuwafukuza wahamiaji haramu.
Trump mara kwa mara amekuwa akisema Marekani imevamiwa na wahuni na wahalifu kutoka mataifa ya kigeni.
Mwezi Februari, Rais Trump aliagiza kufukuzwa kwa karibia wahamiaji 250 wa Venezuela kwenda nchini El Salvador bila ya kufikishwa mahakamani akidai kwamba wahamiaji hao walikuwa sehemu ya magenge ya kihalifu.