Marekani: Utawala wa Trump wawafukuza wahamiaji wanane nchini Sudani Kusini

Migogoro ya kisheria ya utawala wa Trump inayoendelea juu ya sera yake ya kufuwakuza wahamiaji nchini Marekani. Jaji wa shirikisho huko Boston amebaini kwamba Serikali ya Marekani limekiuka moja ya maamuzi yake kwa kuwafukuza wahamiaji kadhaa bila kuwapa muda wa kutosha kukata rufaa. Tatizo ni kwamba tayari wameondoka, kuenlekea nchi ya Afrika.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Washington,Guillaume Naudin

Wako wanane kutoka nchi sita tofauti: Sudan Kusini, Vietnam, Laos, Burma, Mexico na Cuba. Wahalifu wa kutisha na majambazi, watu wenye makosa ya unyanyasaji wa kijinsia, wizi na mauajikulingana na Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani, .

Walifahamishwa Jumanne jioni kwamba watafukuzwa na kwenda Sudani Kusini. Nchi iliyo katika ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, kulingana na taarifa za hivi majuzi za maafisa wa Umoja wa Mataifa. Si muda mrefu, kwa vyovyote vile, kwa jaji kuzingatia kwamba mawakili wao wanaweza kukata rufaa ya kufukuzwa huko. Hatoi muda maalum, lakini jaji anataka wabaki chini ya ulinzi wa mamlaka ya Marekani hadi haki zao ziheshimiwe.

Katika kikao kipya cha Jumatano, aliamua kwamba serikali ilikiuka moja ya maamuzi yake ya hapo awali, ikizingatiwa haswa wakati waliopewa kupinga kufukuzwa kwao “hautoshi,” kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Marekani.

Ndege hiyoinayowabeba inasemekana iko Djibouti

Msemaji wa Wizara ya Usalama wa Ndani Tricia McLaughlin amemshutumu jaji wa shirikisho ambaye aliagiza kusitishwa kwa uhamishaji kwa “kujaribu kulazimisha Marekani kuwarudisha wanyama hawa,” wakati wa mkutano na waandishi wa habari, akisisitiza kuwa wote wamepatikana na hatia ya uhalifu wa kutumia nguvu. “Kuna watu wanane kwenye ndege. “Kwa sababu za kiusalama, hatuwezi kukuwambia hatua yao ya mwisho ya watu hawa itakuwaje,” Tricia McLaughlin amesema akijibu swali kuhusu idadi ya watu waliofukuzwa kwenda Sudani Kusini.

Mamlaka za Marekani zinaeleza kuwa hii ndiyo hali halisi, na kwamba ndege imetua, lakini bado haijafika inakoenda, jambo ambalo hawaelezi. Gazeti la New York Times linabaini kwamba ndege hiyo aina ya Gulfstream V, mojawapo ya ndege za kibinafsi maarufu, kwa sasa iko nchini Djibouti.

Hii si mara ya kwanza kwa mahakama kupinga maamuzi ya utawala kuhusu kufukuzwa kwa wahamiaji, lakini Ikulu ya Marekani imepuuza mara kwa mara maagizo yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *