Marekani: Trump kutangaza ‘hivi karibuni’ asilimia 25 ya ushuru wa forodha kwa bidhaa za Ulaya

Zaidi ya mwezi mmoja baada ya kurejea madarakani, Donald Trump amefanya mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri Jumatano, Februari 26. Katika mkutano na waandishi wa habari, ametoa kauli kadhaa, ikiwa ni pamoja na ushuru wa forodha, mojawapo ya kipaumbele chake kikuu tangu alipochaguliwa tena. Kwa hivyo, bidhaa za Ulaya “hivi karibuni” zitatozwa ushuru wa forodha wa 25%. Pia amerejelea malalamiko yake dhidi ya Umoja wa Ulaya.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza siku ya Jumatano, wakati wa mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri katika Ikulu ya White House, kwamba bidhaa za Ulaya zitatozwa ushuru wa forodha wa 25%. “Tumefanya uamuzi, na tutautangaza hivi karibuni, itakuwa 25%,” amehakikisha Donald Trump, kiwango ambacho bidhaa za Canada na Mexico pia zinapaswa kutozwa ushuru kuanzia mwanzoni mwa mwezi wa Aprili.

“Ulaya iliundwa kuiudhi Marekani”

Lakini juu ya yote, maneno hayaonekani kuwa na nguvu ya kutosha dhidi ya mradi wenyewe wa Ulaya, ambao, kulingana na rais wa Marekani, uliundwa dhidi ya Marekani tangu mwanzo. “Nchi za Ulaya zimetutumia vibaya sana, hazikubali magari yetu, au bidhaa zetu za kilimo, na zinatoa kila aina ya sababu, wakati sisi tunakubali kila kitu kutoka kwao,” Donald Trump amesema.

“Tuna nakisi ya dola bilioni 300 nao, hivyo kwa upande wangu, napenda nchi za Ulaya, lakini Ulaya iliundwa ili kuiudhi Marekani, hilo ndilo lengo na wamefanikiwa hadi sasa, lakini sasa mimi ni rais,” ameongeza.

Umoja wa Ulaya ni “muhimu” kwa Marekani, kulingana na Tume

Majibu rasmi ya Tume yalikuwa ya haraka.

Takwimu hii ya “dola bilioni 300” ya nakisi ya biashara ya Marekani na Ulaya inapingwa na Brussels, ambayo inabaini kwamba inapaswa kupunguzwa kwa nusu. Umoja wa Ulaya ni “muhimu” kwa Marekani, Tume ilimjibu Donald Trump siku ya Jumatano.

“Umoja wa Ulaya ndio soko huria kubwa zaidi duniani. Na ilikuwa ni jambo la mungu kwa Marekani,” amesema msemaji wa taasisi hiyo ya Ulaya katika taarifa kwa vyombo vya habari. Tume ilitoa wito wa “kushirikiana kuhifadhi fursa hizi kwa raia na wafanyabiashara wetu. Sio mmoja dhidi ya mwingine,” maandishi yanaongeza. “Kwa kuunda soko moja, kubwa na jumuishi, EU imewezesha biashara, kupunguza gharama kwa wauzaji bidhaa wa Marekani na kuwianisha viwango na kanuni katika nchi 27 wanachamawa Umoja wa Ulaya,”amebainisha.

“Ulaya itachukua hatua mara moja na kwa uthabiti” anasema Kamishna wa Ulaya anayehusika na Soko la Pamoja, Stéphane Séjourné, anaripoti mwandishi wetu huko Brussels, Pierre Benazet.