“Marekani ni aina mbaya zaidi ya Uistikbari”, andiko jipya kwenye ukurasa wa X wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Akaunti ya mtandao wa X ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya khamenei.ir imetoa mjibizo kwa lugha ya Kihispania yenye hashtag GolfoDeMéxico kujibu hatua ya Marekani ya kulibadilsha jina Ghuba ya Mexico.