
Marekani na China “zitapunguza ushuru wao kwa asilimia 115”, Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva Jumatatu, Mei 12. Washington na Beijing zimefanya mazungumzo ya siku mbili kutafuta suluhu la vita vya forodha vilivyoanzishwa na utawala wa Trump. Wakati wa mapumziko ya siku 90, pande hizo mbili zitajadiliana, amesema Jamieson Greer, Mwakilishi wa Biashara wa Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Kusimamishwa kwa ushuru wa forodha kutaanza “Mei 14,” mataifa makubwa mawili yenye nguvu zaidi ya kiuchumi duniani yametangaza katika taarifa ya pamoja iliyochapishwa baada ya mazungumzo ya siku mbili huko Geneva, ambayo yalifuatiliwa kwa karibu na dunia nzima. Washington na Beijing zinatambua “umuhimu wa uhusiano wa kiuchumi endelevu, wa muda mrefu na wenye manufaa kwa pande zote.”
Pande zote mbili zimekubali kusitisha ushuru wa asilimia 115 walizowekeana katika wiki za hivi karibuni, kama sehemu ya vita vya biashara vilivyoanzishwa mwezi wa Aprili na Donald Trump, ambaye alishutumu uhusiano usio na usawa wa kibiashara kwa China.
Maamuzi haya kwa hiyo yanapunguza kwa muda ushuru wa forodha wa Marekani kwa China hadi asilimia 30 na ushuru wa forodha wa China kwa Marekani hadi asilimia 10, huku mazungumzo kati ya nchi hizo mbili yakiendelea, amesema Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Jamieson Greer katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva.
Kupunguzwa kwa ushuru wa forodha za Marekani kunapaswa kuongeza mauzo ya nje ya China na kuongeza uchumi, kama kutokuwa na uhakika duniani kunazidi, anasema mwandishi wetu wa Beijing, Clea Broahurst. China pia iliahidi kusitisha baadhi ya hatua zisizo za ushuru, hatua inayoashiria nia yake ya kushirikiana na inaweza kuongeza taswira yake katika jukwaa la kimataifa. Lakini nyuma ya utulivu huu, Beijing inaendelea na mkakati wake wa kupunguza utegemezi wake kwa teknolojia na masoko ya Marekani. Njia ya kujiandaa kwa siku zijazo huku ikichukua fursa ya kupunguza mvutano wa sasa.
“Tunataka biashara yenye uwiano zaidi (uhusiano)”
“Hakuna upande unaotaka kusambaratika” kwa uchumi wao, Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent amesema mjini Geneva siku ya Jumatatu. “Tunataka uhusiano wa kibiashara wenye uwiano zaidi,” ameongeza, akiamini kwamba vikwazo vya forodha vilivyoanzishwa katika miezi ya hivi karibuni vilikuwa vimeanzisha “vikwazo” vya biashara kati ya nchi hizo mbili.