
Ni mgawanyiko wa kutisha na wenye vurugu, ambao unavunja uhusiano mzuri wa hapo awali: Donald Trump na Elon Musk wamevunja uhusiano wao. Rais wa Marekani na tajiri mkubwa zaidi duniani wametumia saa chache zilizopita kutukanana kupitia mitandao ya kijamii huku kukiwa na kutofautiana kuhusu bajeti ya Marekani. Donald Trump sasa anatishia kusitisha kandarasi nyingi zinazounganisha serikali ya shirikisho na kampuni za Musk.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kuingia kwenye mzozo na rais wa nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani ni ujumbe mbaya kwa wawekezaji: Hisa ya Tesla ilishuka kwa 14% siku ya Alhamisi, Juni 5, wakati mvutano ulipozuka, kabla ya kupanda kidogo wakati wawili hao walipofanya mazungumo ya simu siku ya Ijumaa, Juni 6, na kwa hiyo upatanisho unaowezekana, ulibainiswa. Bila shaka, bei za soko la hisa ni kama mabadiliko ya hisia wakati kuna dhaifu fulani: huja na kuondoka.
Lakini Gazeti la Washington Post lilifanya hesabu: ukijumlisha misaada, ruzuku, na maagizo ya serikali, makampuni ya Musk yamenufaika na dola Bilioni 38 za pesa za umma kwa miaka 20. Chukua SpaceX, kampuni ya anga ambayo mikataba yake na NASA na Pentagon ni dola Bilioni 22.
Mnamo mwaka, kandarasi hizi na serikali ya shirikisho zilichangia robo ya mapato yake. Lakini utegemezi ni wa pande zote. Programu za anga za juu za Washington, zikiwemo za kijeshi, zingekuwa na wakati mgumu kufanya bila huduma za Elon Musk. Na chochote atakachosema Donald Trump, haitakuwa rahisi kubadili mtindo huo haraka.
Hatari za usumbufu kwa NASA na Pentagon
Mvutano unaonekana kupungua kwa kiasi fulani, lakini NASA inaonekana kuwa mwathirika mkuu wa vita vya wazi kati ya wawili hao. Mpango wa anga za juu wa Marekani ulijikuta katikati ya mzozo huu wa mitandao ya kijamii jana.
Baada ya Donald Trump kutishia kwenye Truth Social kufuta kandarasi za serikali ya Elon Musk, bilionea huyo alitangaza kwenye X kwamba ataondoa chombo chake cha anga cha Dragon, ambacho ndicho pekee chenye uwezo wa kuwasafirisha wanaanga kutoka Marekani hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.
Wakati Elon Musk hatimaye alirudi nyuma saa chache baadaye, hata hivyo alifichua uwezekano wake wa usumbufu. Kulingana na kamanda wa pili wa SpaceX, Gwynne Shotwell, kampuni hiyo ina dola Bilioni 22 katika kandarasi na serikali ya Marekani. Mikataa mingi inahusisha NASA, kupitia chombo cha anga cha juu cha Dragon na mpango wa Artemis, ambao unatarajiwa kuwarudisha wanaanga wa Kimarekani kwenye Mwezi mnamo mwaka 2027.
Lakini sehemu kubwa ya mikataba hii pia inahusu Pentagon. SpaceX huzindua mara kwa mara satelaiti za kijasusi kwa wanajeshi wa Marekani. Na Wizara ya Ulinzi pia imeagiza kampuni hiyo kujenga toleo salama zaidi la mtandao wa satelaiti wa Starlink kwa mawasiliano ya kijeshi.