
Nchini Marekani mshukiwa wa shambulio la mabomu ya petroli (Molotov cocktails) katika maandamano ya amani ya kuunga mkono mateka wa Israeli walioko Gaza, ameshtakiwa kwa “uhalifu wa chuki” na anakabiliwa na kifungo cha maisha. Siku ya Jumatatu, Juni 2, mamlaka huko Colorado, ambapo shambulio hilo lilitokea, walitoa maelezo zaidi juu ya kesi hii, ambayo imezua hisia nyingi, ikiwa ni pamoja na za kisiasa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu nchini Marekani, Loubna Anaki
Takriban saa 24 baada ya kukamatwa, Mohamed Sabry Soliman alifika mbele ya hakimu kwa jumla ya dakika mbili. Hiki kilikuwa kikao cha awali cha kumjulisha kuhusu mashtaka dhidi yake: makosa ishirini, yakiwemo kujaribu kuua na kupatikana na vilipuzi.
Katika mkutano na waandishi wa habari, wachunguzi walieleza kwamba alikiri kila kitu. Kwa polisi, Mohamed Sabry Soliman alieleza kwamba alipanga shambulio hili kwa mwaka mmoja na kwamba ilikuwa ni lazima “kuwaua Wazayuni wote.”
Mamlaka inasisitiza kwamba lengo lake lilikuwa ni kusababisha wahasiriwa wengi iwezekanavyo, kwani mabomu ya petroli kumi na sitaa mbayo hayakutumika yalipatikana akiwa nayo wakati wa kukamatwa kwake.
Shambulio hili bila shaka lilizua hisia kali, huku Donald Trump, msemaji wake, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakitangaza kwamba “chuki hii haina nafasi katika nchi yetu.”
Visa ya utalii
Baadhi ya washirika wa karibu wa rais hawasiti kutumia kesi hii kutaka sera kali zaidi ya uhamiaji. Mohamed Sabry Soliman aliwasili Marekani mwaka 2022 kwa visa ya kitalii kabla ya kuomba hifadhi, ambayo ilikuwa bado inasubiriwa. “Lazima tukomeshe uhamiaji huu wa kujitoa mhanga,” ameandika Stephen Miller, “Waziri wa Uhamiaji” wa Donald Trump.