
Kutoka California kupitia New York hadi Texas, maandamano yamefanyika katika miji mingi ya Marekani kumpinga Donald Trump siku ya Jumamosi, Aprili 5. Maandamano hayo yaliyopewa jina la “Hands Off,” ni maandamano ya kwanza makubwa dhidi ya sera za bilionea huyo wa chama cha Republican tangu arejee Ikulu ya Marekani mnamo Januari 20.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Katika maandamano ya kwanza makubwa ya wapinzani wa Donald Trump tangu kurudi kwake madarakani mwishoni mwa mwezi wa Januari, maelfu ya Wamarekani wameandamana Jumamosi, Aprili 5, dhidi ya sera za rais wa 47 wa Marekani. Kuanzia Boston hadi Houston na kutoka Florida hadi Colorado, vuguvugu kadhaa za raia wa mrengo wa kushoto ziliitisha maandamano dhidi ya kile wanachokiita bilionea huyo wa Republican “kunyakua madaraka.”
Moja ya maandamano makuu yaliyofanyika Washington, kwenye National Mall, eneo kubwa ambalo liko kati ya Capitol na Obelisk hukoWashington. Hadi watu 20,000 – na labda zaidi – walikusanyika hapo, katikati mwa mji mkuu wa shirikisho ambao ni ngome ya Wademocrats, ambao umekumbwa sana na watu kuachishwa kazi kwa utumishi wa umma.
Waandaaji wa maandamano ya “Hands Off” wamelenga kufanya mikutano katika maeneo 1,200, ikiwa ni pamoja na katika majimbo yote 50 ya Marekani. Maelfu ya watu walijitokeza katika miji ya Boston, Chicago, Los Angeles, New York na Washington DC, miongoni mwa miji mingine, siku ya Jumamosi.
Waandamanaji walitaja malalamiko dhidi ya ajenda ya Trump kuanzia masuala ya kijamii hadi kiuchumi.
Siku chache zijazo baada ya tangazo la Trump kwamba Marekani itatoza ushuru wa forodha kwa nchi nyingi ulimwenguni, maandamano pia yalifanyika nje ya Marekani, pamoja na London, Paris na Berlin.