Marekani kuiunga mkono Morocco kuhusu suala la Sahara Magharibi

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio, hapo jana alirejelea tena msimamo wa serikali yao kuhusu kuiunga mkono Morocco na mpango wa kisiasa kwa ajili ya eneo la Sahara Magharibi linalotaka kujitenga na Rabat, jambo ambalo ni kiini cha mzozo na Aligeria.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,Marco Rubio akikutana na waziri mwenza wa Morocco,Nasser Bourita jijini Washington,amesema Marekani inatambua umiliki wa Morocco wa eneo hilo na itaunga mkono mpango wa serikali ya Morocoo wa eneo hilo kujitawala kama njia pekee ya kumaliza mzozo kuhusu eneo hilo.

Aidha Marekani imeeleza matumaini ya mazungumzo kuhusu mpango kumalizika hivi karibuni.

Mwaka 2020 wakati wa utawala wa kwanza wa rais Donald Trump;Marekani ilikuwa imetangaza msimamo huo huo na kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Rabat.

Aidha  Mwaka jana rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron,alitangaza uungwaji mkono wa mpango huo wa eneo hilo kujitawala.

Morocco imekuwa ikimiliki koloni za  zamani za Hispania ila imepingwa na vugugu la Polisaria Front linaloungwa mkono na Algeria,Algeria ikiwa imesitisha uhusiano na Morocco tangu mwaka 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *