
Baada ya Emmanuel Macron,ni zamu ya Keir Starmer, Waziri Mkuu wa Uingereza, ambaye amekwenda Washington siku ya Alhamisi, Februari 27. Keir Starmer pia, anajaribu kumshawishi Donald Trump kwamba amani ya Ukraine haitapatikana bila Kyiv na nchi za Ulaya kushirikishwa.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kwa ziara yake hii huko Washington, vyombo vya habari vya Uingereza vinaiona kama mtihani wa kwanza wa kweli wa kidiplomasia kwa Keir Starmer. Mkutano huu utaweka mkondo wa uhusiano wa siku zijazo kati ya nchi hizo mbili. Na ili kumtuliza mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Uingereza amepanga mambo kadhaa: kabla ya kuzuru ng’ambo ya Atlantiki, alitangaza ongezeko kubwa la bajeti ya ulinzi, iliyodaiwa kwa Bara la Kale na Donald Trump.
Keir Starmer pia alichukua muda kumpigia simu Emmanuel Macron kuelezea ziara yake katika Ikulu ya White House. Kuhusu Ukraine, atasihi – kama rais wa Ufaransa – kwa Ukraine na nchi za Ulaya kuwa sehemu ya majadiliano na Urusi.
“Nataka amani ya kudumu, na siamini kuwa hii inawezekana ikiwa hakuna njia madhubuti ya kuzuia Putin. “Uingereza itatekeleza wajibu wake na wengine, lakini tunahitaji wavu wa usalama wa Marekani,” kiongozi wa chama cha Labour aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatano akiwa kwenye ndege kuelekea Washington. “Sote tunataka amani. Swali ni kuhakikisha kuwa itakuwa amani ya kudumu,” amesisitiza.
Ni mkutano wa pili tu kati ya Keir Starmer na Donald Trump
Keir Starmer angependa kuchukua nafasi ya mwezeshaji kati ya Marekani na Ulaya, lakini pia anatumai kulinda nchi yake kutokana na ongezeko la ushuru ambalo tayari linatishia Umoja wa Ulaya.
Huu utakuwa ni mkutano wa pili tu kati ya Keir Starmer na Donald Trump, viongozi wawili walio na fikra tofauti. Walikula chakula cha jioni pamoja kwa saa mbili mwezi Septemba mwaka uliyopita katika ghorofa ya mgombea huyu wa chama cha Republican huko Manhattan. Keir Starmer alikuwa ameweka dau kila kitu juu yake, bila kupata taabu kukutana na mpinzani wake Kamala Harris.