Marekani: James Boasberg, jaji wa shirikisho katikati ya mzozo na Donald Trump, ni nani?

James Boasberg ni jaji wa shirikisho ambaye alizuia utawala wa Trump kuwafukuza wahamiaji kwenda El Salvador. James Boasberg, ambaye amesema siku ya Ijumaa, Machi 21, kwamba “ameazimia kuweka rekodi sawa,” lazima pia aamue ikiwa rais wa Marekani ana haki ya kutumia sheria ya kipekee ya mwaka 1798 kuhalalisha kufukuzwa kwa wahamiaji hao. Kesi hii inayoonyesha msuguano kati ya mahakama na Ikulu ya White House, ambayo Jaji James Boasberg amekuwa mtu mkuu katika vita hivi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko New York, Loubna Anaki

Azma yake ya kuuwajibisha utawala wa Trump kumemfanya ashutumiwe vikali kutoka kwa kambi ya Republican, hadi kufikia hatua ambayo rais ametaka kutimuliwa kwake. Lakini James Boasberg anakataa kutishwa na anaendelea kuishinikiza serikali ili kujuwa kama kweli au hapana Ikulu ya White House iliwafukuza mamia ya wahamiaji wanaoshutumiwa kuwa wanachama wa genge kwenda El Salvador licha ya marufuku yake.

Akiwa na umri wa miaka 62, jaji huyu anaelezwa kuwa jaji mahiri na wenzake na mawakili ambao wana kesi naye. Na wakati Donald Trump anamshutumu kuwa mchochezi na mwenye msimamo mkali kutoka mrengo wa kushoto, kazi yake ya miaka 30 inathibitisha kwamba amekuwa akifurahia kuungwa mkono na pande mbili.

Jaji ambaye alishughulikia kesi kadhaa zinazohusiana na shambulio la Capitol

Mnamo mwaka 2002, mzaliwa huyu wa Washington aliteuliwa na Rais wa Republican George W. Bush kwenye nafasi ya jaji msaidizi wa Mahakama ya Juu ya Wilaya ya Columbia (DC). Miaka kumi baadaye, mrithi wa Bush Jr. katika Ikulu ya White House, Mdemocrat Barack Obama, ambaye alimteua kama jaji wa shirikisho kwa uthibitisho wa kauli moja kutoka kwa Bunge la Seneti.

Kama majaji wengi wa serikali huko Washington, ameshughulikia kesi kadhaa zinazohusiana na shambulio la Januari 6, 2021, na sio jaji pekee ambaye serikali ya Trump imejaribu kuondoa kesi kwa sababu haikufurahishwa na maamuzi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *